Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

WAZIRI MKUU MSTAAFU CLEOPA DAVID MSUYA ASTAAFU SIASA RASMI, RAIS KIKWETE AMPONGEZA

Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akiwa viongozi wengine wakuu wa serikali chama cha Mapinduzi CCM, akiwemo Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulrahman Kinana (kushoto) katika hafla ya kumuaga aliyekuwa Waziri mkuu wa Tanzania mara mbili katika awamu mbili tofauti, Mzee Cleopa David Msuya (wa kwanza kulia kwa Rais) ambaye amestaafu rasmi siasa baada ya kuitumikia kwa zaidi ya miaka 33.

Katibu wa CCM, wilaya ya Mwanga, akisoma historia fupi ya Mzee Msuya kabla na baada ya kujiunga na siasa

Baadhi ya Wananchi waliohudhuria hafla hiyo iliyofanyika katika Ofisi za CCM wilaya ya Mwanga

Mjumbe wa Halmashauri kuu wa CCM wilaya ya Mwanga, Joseph Thadayo akitoa salamu za marafiki na wasomi waishio nje ya Mwanga, ikiwemo salamu za Mwanasiasa maarufu na mdhamini wa CCM, Mzee Peter Kisumo ambaye aliwahi kufanya kazi pamoja na mzee Msuya katika Siasa.

Mzee Msuya akitoa pongezi zake kabla ya kuaga rasmi.


Kundi la wazee wa kimila wakiongozwa na Mzee Kasim Msemo wakimkaribisha Mzee Msuya kijijini

Rais Kikwete akizungumza na wananchi katika hafla ya kumuaga Mzee Msuya katika ulingo wa siasa, uliofanyika katika ofisi za CCM wilaya ya Mwanga.

Mamia ya Wananchi waliokusanyika kushuhudia hafla hiyo


Picha zote na Dixon Busagaga wa

Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO