Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Umoja wa katiba ya wananchi-UKAWA- wamekutana Zanzibar na kutoa tamko la kuikataa Hati ya Muungano kuwa ni batili na hawana mpango wa kurudi Bungeni hadi kieleweke.

_MG_9770

Viongozi wa UKAWA wakiwa katika mkutano na Waandishi wa habari katika ukumbi wa hoteli ya Mzsons Shangani Zanzibar baada ya mkutano wao kuahirishwa na jeshi la Polisi Zanzibar kwa sababu za kiusalama .

Mwenyekiti wa Chama cha CUF Mhe. Profesa Lipumba akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kutoka kwa Wajumbe wa UKAWA kutoka Vyama vya Upinzani Wanaohudhuria Bunge Maalum la Katiba

 

Mwenyekiti wa  CHADEMA, Mhe. Freeman Mbowe, akizungumza na waandishi wa habari sababu za kutoka katika bunge maalum la katiba Tanzania.akisisitiza jambo katika mkutano huo uliofanyika ukumbi wa hoteli ya Mazsons shangani Zanzibar.

Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Mhe. James Mbatia akizungumza na waandishi katika ukumbi wa hoteli ya Mazsons Zanzibar.

Baadhi wa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wa UKAWA waliotoka katika Kikao cha Bunge hilo wakiwa katika ukumbi wa hoteli ya Mazsons Shangani Zanzibar wakizungumza na waandishi wa habari.

Baadhi wa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wa UKAWA waliotoka katika Kikao cha Bunge hilo wakiwa katika ukumbi wa hoteli ya Mazsons Shangani Zanzibar wakizungumza na waandishi wa habari.

 

*********************************************

Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ATAHADHARISGA Kero za Muungano hazitoweza kupatiwa suluhisho endapo mchakato wa Katiba mpya utakwama

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akilifunga Kongamano la Maadhimisho ya Muungano wa Tanganyika  na Zanzibar kutimia miaka 50 lililofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort  Mazizini Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Baadhi ya Washiriki wa Kongamano la Maadhimisho wa Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar lililofanyika Zanzibar Beach Resort na kushirikisha watu wa Taasisi na Jumuiya tofauti za Elimu,Dini, Siasa na Utamaduni Nchini.

*******************************************************************

 

Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi na Mjumbe wa Bunge la Katiba, Profesa Ibrahim Lipumba akisalimiana na wananchi kwenye Viwanja vya Kibanda Maiti Zanzibar jana, baada ya kuwasili Visiwani humo kwa ajili ya mkutano wa hadhara ambao haukufanyika baada ya Jeshi la Polisi kuzuia. Picha na Emmanuel Herman

SOURCE: HAKI NGOWI.COM

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO