Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

HATIMAYE DAVID MOYES ATIMULIWA MANCHESTER UNITED; GIGGS KOCHA WA MUDA

David-Moyes

Mkufunzi mkuu na meneja wa klabu ya Manchester United David Moyes ametimuliwa.

David Moyes amefutwa kazi baada ya kushikilia usukuni wa klabu hiyo kwa miezi kumi tu.

Moyes, mwenye umri wa miaka 50, aliteuliwa na Ferguson kumrithi alipostaafu mwaka jana baada ya kuwa na klabu hiyo kwa miaka 26.Klabu hiyo hapo awali ilikuwa imekataa kuzungumzia udaku wa magezti kuwa Moyes atafutwa kazi kabla ya msimu kumalizika.

Taarifa kutoka kwa klabu hiyo imemshukuru Moyes kwa bidii, uaminifu na hekima aliyoonyesha kocha huyo akiwa mkufunzi wa Manchester United.

Moyes alichukuwa usukani wa kuifunza Manchester United mwaka uliopita baada ya aliyekuwa kocha wa siku nyingi Sir. Alex Ferguson kustaafu.

Huku zikiwa zimesalia mechi nne pekee msimu wa ligi kukamilika Mancheseter united inashikilia nafasi ya saba kwenye jedwali la msimamo wa ligi hiyo alama ishirini na tatu nyuma ya viongozi Liverpool.

Klabu hiyo imeshindwa kufuzu kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa ulaya kwa mara ya kwanza katika kipindi cha takriban miaka ishirini.

CHANZO: BBC SWAHILI.

***************************************

 

Kocha wa muda wa Man united Ryan Giggs akiwasili Carrington asubuhi ya leo tayari kwa kuongoza mazoezi kwa mara ya kwanza

Posted by JAFE JACKSON at Tuesday, April 22, 2014

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO