Wakazi wa eneo la Mapinga Mkoani Pwani wameshindwa kuvuka Daraja la Mto kwenda na Bagamoyo au Dar, unaokatisha kwenye eneo hilo baada ya kutokuwepo kwa mawasiliano ya barabara kwa kukatika kwa daraja hilo kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha hivi sasa katika maeneo mbali mbali hapa nchini.
Akithibitisha kutokea kwa hitilafu hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, ACP Ulrich Matei amesema ni kweli kumetokea kwa tatizo hilo na amewataka watumiaji wa barabara ya Bagamoyo kubadilisha njia na kuwanza kutumia barabara ya Morogoro mpaka hapo daraja hilo litakapofanyiwa matengenezo, matengenezo ambayo tayari yamekwishaanza.
Mawasiliano kati ya Dar na Bagamoyo kwa barabara ya Bagamoyo yamekatika. Maji yanayopita katika mto Mpigi ambako daraja halipitiki ni mengi sana kiasi kwamba nguzo tatu zinazopitisha umeme mkubwa kwenda Bagamoyo zipo hatarini. Mojawapo maji yanaikaribia zaidi na uwezekano wa kusombwa ni mkubwa kwa sababu miti mikubwa iliyokuwa karibu na eneo hilo nayo imeng'olewa kirahisi kabisa.
Picha: Abel Ngapemba; Father Kidevu Blog
0 maoni:
Post a Comment