Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

ZITTO ZUBERI KABWE NA HATIMA YA KISIASA KUTOKANA NA ULEVI WA KIVULI CHA UMAARUFU TANZANIA.

 

NA DANIEL EZEKIEL DANIEL.

kabweZITTO ZUBERI KABWE ni miongoni wa vijana wenye uwezo mkubwa sana wa kufikiria,kuchambua,kutegua mitego,kuchukua hatua na pengine kwa kasi yenye weledi mkubwa hasa katika siasa.

Zitto Kabwe katika historia yake,historia inamuonesha Zitto kabwe aliweza kuwa miongoni mwa vijana waliokuwa smart katika utetezi wa wanafunzi katika chuo kikuu cha Dar es Salaam( UDSM) mwanzoni mwa miaka ya 2000's kupitia uwanja wa zaidi ya MAPINDUZI( Revolution square) kama jukwaa lililoluwa mahala pa kutetea maslahi ya wanafunzi na watanzania kwa ujumla chuoni hapo.

Mwaka 2004,Freeman Aikael Mbowe alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa CHADEMA taifa na Mbowe alitaka kufanya transformation kubwa sana ya CHADEMA. Alitaka kubadilisha mifumo ya uendeshaji wa CHADEMA, alitaka kubadilisha nembo za CHADEMA na kubwa kuliko yote alitaka vijana wapewe nafasi katika chama ngazi za wilaya,mikoa na taifa hasa makao makuu.

Katika mpango wake huo,Mbowe alianza kufanya ziara chuo kikuu cha Dar es Salaam na kuangalia vijana machachari ,jeuri,wazungumzaji na makini.Mbowe aliona na kuridhishwa na vijana kama vile Halma Mdee,Zitto Kabwe,John Mnyika,John Mrema na baadaye David Silinde,Daniel Naftal,Owawa,Juliana Shonza,Mtela mwampamba,Burton Gwakisa Mwakasendo nk .

Mbowe aliweza kuwaomba na kuwashawishi kujiunga na CHADEMA. Zitto Kabwe pia alijiunga CHADEMA mwaka 2004 na siyo mwaka 1993 akiwa na miaka 16 kama anavyojitapa.John Mnyika yeye alikaa bila kadi ya CHADEMA mwaka mzima yaani tangu 2004 na kujiunga rasmi kwa kuchukua kadi mwaka 2005 alipokuwa anataka kugombea ubunge.

Licha ya Mbowe kuomba vijana kujiunga na CHADEMA, Mbowe pia aliendelea kushawishi wazee na wanawake kutoka vyama Vinginevyo vya siasa,asasi za kiraia,taasisi za dini nk.Mifano ni mingi,Tundu Lissu aliombwa kuhamia CHADEMA kutoka chama cha NCCR MAGEUZI, Mabere Marando Aliombwa kujiunga CHADEMA kutoka NCCR MAGEUZI,Prof Abdallah Safari aliombwa kutokea CUF,Peter Msigwa aliombwa kutoka ccm na wengine wengi.Mbowe aliwapa uhuru vijana na wazee hawa kufanya siasa dhidi ya ccm.KIPINDI HIKI NI WAKATI CUF,NCCR NA CHADEMA HAVINA USHIRIKIANO WOWOTE KAMA ILIVYO SASA UKAWA.KWA SASA KUSHAWISHI WANACHAMA WA CHAMA KIMOJAWAPO CHA UKAWA NI KOSA KUBWA ,HAIRUHUSIWI.

Baada ya vijana kwa wazee kupewa nafasi katika chama,vijana walifanya kazi.Zitto Kabwe alifanya siasa nzito na yenye weledi mkubwa sana mwaka 2004/2005.

Mwaka 2005,Zitto alikua ameiva sana kisiasa.Alikuwa tayari akilitaka jimbo la Kigoma kaskazini kupitia chadema.Mnamo Julai 2005 Zitto Kabwe alivishwa suti nzito na ya Kupendeza na Mbowe katika mkutano mkubwa wa Hadhara uliofanyika mwembe Yanga Jijini Dar es Salaam.

Ninayasema ya kuvishwa Suti kutokana na Zitto kabwe alikuwa ni kijana aliyeshikilia misimamo ya kisoshalisti( Socilist ideology) au itikadi za kijamaa hivyo aliiga hata mavazi ya wasosholojist nguo za kawaida,nguo za kubana sana na nguo zisizo na thaman sana.Zitto alipotangaza nia ya kugombea ubunge kigoma kaskazini,Mbowe alisema " ili uwe mbunge na uwe na sura ya kibunge,vaa nguo hizi kamanda,tuelekee kigoma".Zitto alivaa suti zile na maelfu ya watu walimshangilia sana.Mbowe alichukua Helkopta yake pamoja na Zitto Kabwe wakaelekea kule kigoma.


Zitto Kabwe alipigana na akapiganiwa akashinda jimbo na kuwa mbunge wa kigoma kaskazini kupitia CHADEMA. Zitto akiwa Mbunge ,Dk Slaa pia alikuwa mbunge.Dk Slaa kwa weledi wake na umakini,alimpa hoja Zitto Kabwe ya Mgodi wa Buzwagi na akamwambia chama kitakutetea kwa ushahidi.

Zitto alisimama bungeni na kujenga hoja yake akijua kabisa wapo watu nyuma yake.Na kwa uwezo wake mkubwa wa ushawishi,uwezo mkubwa wa kuwasilisha hoja,uwezo mkubwa wa kuwa na mvuto kisiasa,Zitto alifanikiwa to CULPTURE MIND ZA WATU WENGI SANA NDANI YA BUNGE NA NJE YA BUNGE.Sitta aliomba kuzima hoja hii haraka,Zitto akafukuzwa bungeni,ilikuwa Julai 2007.

Zitto hapo akapata Umaarufu wenye hashima kubwa.Zitto akawa ni Mwanasiasa kijana mwenye weledi na kupendwa na watanzania. Zitto na Dk slaa waling'ara zaidi hasa baada ya Dk slaa naye kutaja orodha ya mafisadi(LIST OF SHAME) wa taifa hili tarehe 15/09/2009 katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es Salaam.

Wakati bado Zitto akiwa katika chati hiyo kubwa,Zitto aliweza kuwekwa mstari wa mbele kuongoza OPERATION ZA CHADEMA mwaka 2007,2008 na 2009 ambapo Zitto alikuwa mstari wa mbele katika OPERATION SANGARA KANDA YA ZIWA,OPERATION KATIKA MAJIMBO KADHAA YA UCHAGUZI MDOGO KAMA VILE BUSANDA,TARIME NA MBEYA VIJIJINI.

Mwaka 2008 novemba tarehe 23 Zitto Kabwe akiwa Mbalizi Mbeya,alinipa kadi ya CHADEMA na nikajiunga rasimi CHADEMA hasa baada ya zitto kabwe kutoa Speech Kali sana Mbalizi kuhusu jinsi Rais Kikwete alivyowatesa vijana wa chunya waliompiga mawe katika ziara yake.Zitto alisema " Kikwete aliamuru vijana wote Kijiji kile wakamatwe na walipokamatwa waliwekwa kwenye maji ya barafu na korodani zao zilipigwa kwa rula hali ambayo iliniumiza na nikaamua kupambana vijana wale 8 wakatoka".Speech hii ya zitto kabwe ilinitoa machozi na ndipo nikajiunga na CHADEMA na ninakumbuka Wananchi tulisukuma gari ya Zitto kutoka ZZK Mpaka Daraja la reli pale mbalizi.

Katika hali isiokuwa ya kawaida,Mwezi Agost 2009,Zitto akalewa sifa sana.Akajiona sasa yeye ni zaidi ya mbowe,ni zaidi ya CHADEMA, ni zaidi ya Dk slaa na akajiona ni zaidi ya yeyote ndani ya CHADEMA. Akatangaza kupambana na mbowe katika kuwania nafasi ya uenyekiti wa CHADEMA TAIFA. Wazee wa CHADEMA wakamwambia,asubiri Mbowe amalizie miaka 5 ndipo agombee naye.Zitto akakubali kwa shingo upande na Mbowe akawa mwenyekiti na kumteua Zitto kabwe kuwa Naibu katibu mkuu bara.


Zitto Kabwe mwaka 2009 hakufanya kazi yoyote makao makuu kama naibu katibu mkuu.Alikua bize na kazi zake kwa kile alichosema " ana andaa jimbo lake la kigoma kaskazini ili ashinde zaidi.".Zitto akawa rafiki wa Karibu kwa kikwete .

Mwaka 2010,Zitto alianza kugoma kushiriki kazi za chama bali akawa bize sana na kile alichokiita majukumu ya kibunge.Zitto yule wa 2007,2008 akawa na sura ya uhapana,undio na sura ya siko tayari.Operation za CHADEMA hasa maandalizi ya uchaguzi mkuu akawa very Inactive kama sio passive.Zitto akawa ni mtu wa safari za nje ya nchi kila wakati.

Uchaguzi mkuu ulipokaribia,Dk slaa alipata ajali ya kuanguka aliopokua akioga,aliyepaswa kukaimu nafasi yake ni Zitto Kabwe.Zitto hakuwepo nchini na John Mnyika akakaimu nafasi ya Katibu mkuu.

Zitto kabwe aliporejea,alimkuta John Mnyika,akamwambia,ondoka,mimi ndiye mkubwa wako.John Mnyika alikuwa mkurugenzi wa mawasiliano,uenezi na itikadi kipindi hicho.Mnyika alikubali kumuachia ofisi Zitto.

Badala ya zitto kabwe kufanya kazi za chama akaanza kuharibu.Majimbo yaliyotoa wagombea na tayari walipitishwa kuwa wagombea kwa udhamini wa CHADEMA, Zitto aliwaagiza wagombea wa CHADEMA kujiondoa na wale waliogoma aliwaondoa kwa nguvu yeye kama naibu katibu mkuu na kwa muda huo kama kaimu katibu mkuu.

Majimbo aliyoondoa wagombea wa CHADEMA ni pamoja na jimbo la waziri mkuu Mizengo  Pinda,Musoma vijijini kwa Nimrodi Mkono nk.Huu ni usaliti wa wazi wazi alioifanya zitto kabwe kwa chama.

Mwaka 2010/2011 Zitto akaanzisha kikundi cha vijana wafuasi wake ndani ya CHADEMA badala ya falsafa,itikadi na madhumuni ya CHADEMA.

Zitto akawanoa vijana kama Ben Saa Nane,Habib Mchange,Burton Gwakisa Mwakasendo,Juliana Shonza,Joseph Kasambala,Mtela Mwampamba na wengine kama Prof Kitila Mkumbo,Samson Mwigamba,John Shibuda nk kuwa wafuasi wake na kuasi CHADEMA.

Vijana na hao wengine walifanya kazi usiku na mchana.Walipanga mipango yao ya gizani na nuruni.Walipanga jinsi ya kuangamiza CHADEMA.

Mwaka 2011 katika uchaguzi mdogo wa Igunga,Zitto Kabwe alishiriki kwa Mbinde sana.

Uchaguzi mdogo wa 2012 Arumeru mashariki,Zitto aliwenda siku 2 tu na kuondoka wakati wenzake waliweka kambi kule.Zitto akasema yeye yuko bize na bunge.

Mwaka 2012 hiyo hiyo,Mwezi Aprili,CHADEMA ilizindua OPERATION ILIYOJULIKANA KAMA VUGUVUGU LA MABADILIKO YAANI MOVEMENT FOR CHANGE( M4C) Zitto Kabwe kama naibu katibu mkuu hakuhudhuria uzinduzi huo na alipoulizwa akasema alikuwa Marekani kichama kufungua matawi ya CHADEMA Diaspora.

Mwenzi mei na Juni,Operation ya m4c Lindi na mtwara,wabunge wote na viongozi waandamizi wa CHADEMA makao makuu walielekea mtwara na Lindi lakini Zitto hakujihusisha kabisa.

Katika mtando wa Jamii Forum,Zitto alitoa nafasi kwa watu mbalimbali kumuuliza maswali.Kuna mwanajamii Forum mmoja alimuuliza Zitto " Je una mpango wowote wa kujitoa CHADEMA au kuanzisha chama chako maana unaonekana uko mbali sana na mipango ya CHADEMA na kazi za chama?".Zitto alijibu kwamba," Sina mpango wowote kuondoka CHADEMA kwa kuwa nimekitumikia CHADEMA kwa muda mrefu sana,nitakuwa CHADEMA mpaka mwisho.CHADEMA ina damu yangu,CHADEMA ina jasho langu.Nitakuwa CHADEMA daima na kuitenga CHADEMA na Zitto CHADEMA itatetereka.".Kwa maneno hayo ya Zitto utagundua kwamba,Zitto anaamini kwamba,kama yeye akiondoka CHADEMA, chadema kitatetereka na hatimaye kufa.Kwa tafsiri rahisi zitto ni zaidi ya CHADEMA, na bila zitto hakuna CHADEMA.

Mwaka 2013 vijana wa Zitto kabwe akina Juliana Shonza( Makam mwenyekiti BAVICHA Bara),Mtela Mwampamba,Gwakisa Mwakasendo,Greyson Nyakarungu,Habib mchange na wengine walipatikana na hatia na baraza la vijana CHADEMA liliwavua uanachama Juliana Shonza,Mtela Mwampamba na Habib Mchange huku Gwakisa Mwakasendo( aliyekuwa msomaji wa GPS ya Helkopta ya Dk Slaa wakati wa kampeni 2010),Joseph Kasambala kupewa onyo kali sana na kusimamishwa.Vijana hawa walilalamika kwamba baada ya wao kufukuzwa CHADEMA, Zitto aliwapuuza na walimripoti na kusema ni mnafiki kwao.Nape naye alisema wanamsubiri Zitto kabwe baada ya vijana wake kushindwa.

Wakati huo huo,Mbowe alidhalilishwa bungeni, wabunge kama Joseph Mbilinyi walipokomaa bungeni, Zitto akasema hakwenda bungeni kupigana.Aliwakashifu wabunge wenzake.

Mwaka huo huo 2013 tarehe 15/6 Wabunge wengi walikua field kwenye uchaguzi mdogo wa udiwani.Bomu lilirushwa na kulipuka kwenye mkutano Arusha huku Mbowe na Lema wakinusurika.

CHADEMA iliagiza wabunge wote wa CHADEMA kwenda kwenye mazishi ya watu waliofariki .Zitto alipotelea kusikojulikana,hakuwepo ARUSHA wala bungeni. Hii nayo ilishangaza wengi.

Mwishoni mwa Disemba 2012 ,Mwigulu nchemba akiwa na Zitto kabwe Star tv tuongee asubuhi,Mwigulu alisema CHADEMA ni magaidi na ana ushahidi.Zitto hakuonesha makali sana kukanusha kauli hiyo.

Baada ya muda si mrefu,Wilfred Rwakatare( Mkurugenzi mkuu wa idara ya ulinzi na usalama wa CHADEMA) alikamatwa kwa kosa la kwamba ni Gaidi.Zitto kabwe haraka haraka aliandika barua kwenda kwa katibu mkuu akitaka Rwakatare atoswe kwa kuwekwa pembeni kwa kile kilochoitwa kupisha uchunguzi huku Zitto akiiweka barua hiyo mtandaoni ,Facebook na Jamii Forum kupitia vibaraka wake au yeye mwenyewe.

Hoja hiyo ilipingwa vikali kwani hapo ndipo makao makuu ilipotoa kauli kwamba kipindi hiki tunatakiwa kuwa pamoja kuliko kipindi kingine chochote katika maisha ya CHADEMA. Zitto alinyong'onyea sana.CHADEMA iliposhinda,alihuzunika zaidi hasa kupitia mawakala wake waliokuwa wamebaki akina Shibuda na ndio maana wakaagiza Henry Kilewo na wenzake kukamatwa,kuteswa na Shibuda na usalama wa taifa kulazimisha akina Kilewo kusema Mbowe na Dk Slaa ni magaidi.Hata hivyo,kesi hii nayo CHADEMA ilishinda.

Mnamo Mwezi Septemba 2013 waraka wa mwenendo wa Zitto Kabwe ulivujishwa na kuwekwa mtandaoni na Henry Kilewo.CHADEMA kupitia kwa mkurugenzi wa Mawasiliano,itikadi na uenezi John Mnyika iliukana waraka huo.

Baada ya mwezi mmoja baadaye ,Novemba ,2013 CHADEMA ilibaini mpango mchafu wa zitto Kabwe,Kitila mkumbo na Samsoni Mwigamba wa kumpindua Mwenyekiti wa CHADEMA TAIFA Mheshimiwa Mbowe.

Waraka wa mpangp huo mchafu kinyume na katiba ya CHADEMA ulimtia hatiani zitto kabwe,Samson Mwigamba na Prof Kitila mkumbo ambao walivuliwa nyadhifa zao.

Zitto kabwe akatafuta vijana na wazee nchi nzima,akiwapa pesa za kutoa matamko na kujivisha vyeo vya CHADEMA huku wakitukana chama na kudhalilisha viongozi wa CHADEMA. Nakumbuka tarehe 25/11/2013 vijana waliojiita viongozi katika vyuo vikuu hasa UDSM na ardhi walitoa tamko kwamba wao ni Vijana wa vyuo vikuu na wakataja vyeo huku wakiwa waongo.Mmoja alijitambulisha kwamba ni katibu wa Chaso udsm huku Karibu wa CHASO udsm nilikuwa mimi.Hii ilipelekea kutoa tamko kukanusha tamko la kupinga maamuzi ya kamati kuu kumvua nydhifa zitto kabwe na wenzake.Matamko yalikuwa mengi sana na yalifadhiliwa na Zitto kwa ushirika wa usalama wa taifa na ccm.

Baada ya kufukuzwa Kitila na Mwigamba,Zitto aliweka Court injuction kujadili uanachama wake Mpaka kesi ya msingi isikilizwe.

Nakumbuka tarehe 3/1/2014 mahakama kuu,Zitto aliandaa vijana mateja waliovalia t.shirt za CHADEMA mpya ambazo zingine hata rebo zilikuwa hazijatolewa huku wakiwa na mapanga,sindano ,Dispiss na wakiwa katika hali mbaya ukiachilia t.shirt mpya.Suruali na pensi zao zilikuwa chafu sana huku wakivaa ndala zenye rangi tofauti au yeboyebo tena zilizoisha sana.Vijana hao  walilipwa na zitto.Wao walikuwa na wimbo wa Zitto kwanza,CHADEMA baadaye.

Hapa ndipo tukiwa na vijana kama Manawa Bukwimba,Daniel Ezekiel,Hilda Newton,Neema Mathias,Baraka Mfilinge,Ben Saanane,Philipo Mwakibinga nk tulianzisha msemo wa "Wafia chama" kama ishara ya ku counter attack kauli ya "Zitto kwanza chama baadaye'.Nakumbuka siku hiyo mapigano yalikuwa makali sana kati ya wafia chama na Zitto Kwanza chama baadaye. Mapigano yalihusisha ngumi,marungu ,mawe na silaha zilizoandaliwa na vijana wa zitto.Diwani wa Ubungo Boniface Jacob aliwadhibiti vikali mateja wale licha ya kuwa na silaha huku sisi tukijilinda dhidi ya mawe na silaha kwa kupambana vikali.

Hali hii ilipelekea jeshi la polisi kutawanya kwa mabomu na risasi za moto na siku hiyo nilipoteza pesa zangu shilingi laki tatu na elfu saba( 307000) wakati wa Mapambano hayo makali.

Nimelazimika kuandika historia hii fupi japo ni ndefu ili watu wajue kwamba Zitto ni mtu aliyelewa sifa na umaarufu na hivyo kuwa msaliti akidhani kwamba bila yeye hakuna harakati za CHADEMA.

Ni kweli Zitto ana ushawishi japo kwa sasa ni kidogo sana ila ni mwanasiasa mwenye bei.Zitto pamoja na kwamba ana mvuto wa kisiasa,msomi na mwenye uwezo mkubwa wa kujenga hoja,lakini Zitto ni msaliti na ana chembechembe za kupoteza wenzake katika mstari.Amepoteza vijana kama Juliana Shonza,Mtela Mwmpamba,Habib Mchange,Greyson Nyakarungu na wafuasi wengine wengi.

Zitto kinachomponza ni usaliti,dhihaka kwa wenzake,Ulevi wa umaarufu,kujiona ni zaidi ya chama,hujuma kwa chama na sasa ni mipango michafu kwa chama huku akisahau kwamba ccm inammaliza kisiasa.Atakuja kukumbuka wakati ccm wameshampoteza katika ramani ya siasa na hivyo kutumika kama TOILET PAPER KAMA SIO MPIRA KATIKA MECHI YA UWANJANI UNAOCHEZWA USIKU AGHARABU.

Mwandishi ni

Daniel Ezekiel Daniel

Mwanasiasa undergound na mchambuzi wa sisa( political Scientist)

danielezekiel2222@gmail.com
0787359776

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO