Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mradi wa Ujenzi Barabara ya Arusha-Holili /TAVETA –VOI Kilometa 122 pamoja na Arusha –bypass (km 42) Unaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB)Wazinduliwa Jijini Arusha

tanroad

Mkurugenzi Mkuu wa wakala wa barabara (TANROADS) ,Injinia Patrick Mfugale akizungumza katika uzinduzi wa mradi wa Arusha-Holili /TAVETA –VOI kilometa 122 pamoja na Arusha –bypass (km 42) unaofadhiliwa na benki ya maendeleo ya Afrika (ADB)uliyofanyika  jijini Arusha

IMG-20140625-WA0045-1Mkuu wa Mkoa Arusha Magessa Mulongo akiongea katika uzinduzi huo

IMG-20140625-WA0040Mwakilishi wa benki ya maendeleo ya Afrika (ADB), Injinia Patrick Musa

20140624_214539Kulia Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema katikati Mkuu wa Wilaya ya Arusha John Mongela na mkurugenzi wa jiji  la Arusha

20140624_222604Washiriki katika uzinduzi huo

20140624_222551

IMG-20140625-WA0042

IMG-20140625-WA0039Meja Stepher Mtaheba wa kikosi cha jeshi  akijitambulisha katika uzinduzi huo

IMG-20140625-WA0038IMG-20140625-WA0043

 

Mkurugenzi Mkuu wa wakala wa barabara (TANROADS) ,Injinia Patrick Mfugale ameshiriki katika uzinduzi wa mradi wa Arusha-Holili /TAVETA –VOI kilometa 122 pamoja na Arusha –bypass (km 42) unaofadhiliwa na benki ya maendeleo ya Afrika (ADB) uliofanyika katika ukumbi wa naura springs mjini hapa.

Alisema kuwa,kumekuwepo na changamoto kubwa sana zinazosababishwa na wananchi na baadhi za halmashauri katika utekelezaji wa miradi hiyo hali ambayo imekuwa ni kikwazo kikubwa katika kufikia malengo yaliyowekwa.

Halmashauri mbalimbali nchini kwa kushirikiana na wananchi wametakiwa kutoa ushirikiano wa kutosha katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuweza kukamilika kwa wakati uliopangwa.

Aidha kumekuwepo na changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikikwamisha miradi hiyo ikiwemo ya wananchi kukataa kulipwa fidia kwa taratibu za sheria za nchi ili kutoa maeneo ya kuchimbwa changarawe, kokoto na kuchota maji.

Alifafanua kuwa, halmashauri za wilaya pamoja na serikali za vijiji wamekuwa wakitoza kodi mbalimbali kwa vifaa vya ujenzi kama kifusi, mchanga,kokoto,na maji.

Mfugale alisema kuwa,mradi wa ujenzi wa barabara ya Arusha-holili ni sehemu ya mradi wa kimataifa unaojulikana kwa jina la Holili/Taveta –Voi unaounganisha nchi yetu na nchi jirani ya Kenya utagharimu kiasi cha dola za kimarekani milioni 223.

Alisema kuwa, awamu ya kwanza ni kuijenga kwa njia nne sehemu ya barabara kutoka Sakina –Tengeru (km 14.1) na Arusha bypass (km 42) kwa fedha za mkopo kutoka ADB .

Aliongeza kuwa, sehemu ya pili ni kuendeleza ujenzi wa njia nne kutoka Tengeru hadi Usa river (km 8.2) na ukarabati wa sehemu ya barabara iliyobaki hadi Holili baada ya kupata fedha.

Naye Mwakilishi wa benki ya maendeleo ya Afrika (ADB), Injinia Patrick Musa alisema kuwa kumekuwepo na changamoto kubwa ya hali ya hewa ambayo imekuwa ikichangia mradi kukamilika kwa wakati na ucheleweshaji wa ulipwaji wa fedha za wakandarasi .

Alisema kuwa, wao kama benki ya maendeleo ya Afrika wataendelea kutafuta hela kwa ajili ya maendeleo kwani ni fursa nzuri wao kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kuleta maendeleo.

Naye Mkuu wa mkoa wa Arusha , Magesa Mulongo aliwataka watekelezaji wa mradi huo kuwajibika ipasavyo ili kuwezesha mradi huo kukamilika kwa wakati.

Aidha Mulongo aliwataka watekelezaji wa mradi huo kuwa waangalifu na waaminifu katika kufanikisha mradi huo huku wakikemea vikali tabia ya wizi wa vifaa vya ujenzi ambavyo vimekuwa vikikwamisha mradi huo.

 

TAARIFA YOTE KWA HISANI YA JAMII BLOGU

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

2 maoni:

Unknown said...

Nyie mnaona wizi 2 je?khaki za wafanya kaz

Unknown said...

hatujakupata vizuri, ni jambo gani unalozungumzia?

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO