Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

ABBAS MTEMVU ATEMBELEA WAATHIRIKA WA MVUA JIMBONI KWAKE TEMEKE

 

Mtemvu akiitembelea Nyumba ya Bi Mwashamba Mwandoro maeneo ya Kurasini,  baada ya ukuta wa Nyumba kuanguka kutokana na Mvua zinazo endelea kunyesha Dar es Salaam na hapo akiongea akiwa katika nyumba hiyo, katika msafara huo aliongozana na Meya na Naibu Meya wa Temeke ,na Diwani wa maeneo hayo.

Mbunge wa Jimbo la Temeke na Mbunge wa Wabunge Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu (kulia) akiongozana na Meya wa Temeke Maabad Suleimani (kati) na Naibu Meya wa Jimbo hilo Juma Mkenga  wakati wa ziara ya  kutembele walio athirika na Mvua zinazoendelea kunyesha

  Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtevu akiyapima maji kwa kuingia katika dimbwi lililokuwa limejaamaji na kumlazim kushuka katika Gari alilokuwa amepanda na kumsaidia Dereva wa Gari  lenye usajili T 526 DDR lililonyuma ya Mbungehuyo kushindwa kupita na baada ya kufanyahivyo dereva huyo alionyeshwa njia ya kupita na kuendelea na safari ni baada ya mbunge huyo kuwa katika Ziara ya kuwatembelea waadhirika wa Mvua.

  Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu akimsaidia kumuelekeza Dereva wa Gari T 526 DDR baada ya uonekana kusuasua na akiwa anaziara ya kuwaona waadhirika wa Mvua

Maji ya Mvua yakiwa yamezingira Nyumba maeneo ya Wailesi Temeke

Mjumbe wa Shina kupitia Chama cha Mapinduzi(CCM)  Juma Salum  (wakwanza kishoto) akitoa maelezo kwa Mbunge wa Jimbo hilo mara alipofika kuwaona


Mtaa mzima ukiwa umefurika maji maeneo ya Wailesi kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha Jijini Dar es Salaam

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Abdon Kidege, akimwelekeza jambo Mbunge wa Jimbo hilo Abbas Mtemvu wakati wa ziara ya kutembelea na kuwaona wananchi waliopatwa na mafuriko ya Mvua zinazo endelea kunyesha

Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu akizungumza na wananchi walio patwa na mafuriko maeneo ya Wailesi alipo watembelea

Madereva wa Magari ya Abiria yanayo fanya safari kati ya Tandika - Yombo Kilakala kupitia Daraja la Tazara na Tandika kwa Limboa wakishirikiana kujaza viroba vya mchanga na kuweka sehemu yamaeneo ya  Barabara hiyo ili waweze kupita kwa urahisi     

Madereva hao wakiwa wanapakia mchanga kwa kuweka katika maeneo nkorofi ambayo yanasababishwa.

Magari yakipita kwa shida na eneo hilo linauterezi kitu ambacho ni hatari sana kwa wanao tumia njia hiyo

Magari mengine yalazimika kushushia katikati ya Daraja kitu ambacho ni hatari na wengine kupata nafasi ya kuosha Pikipiki zao


Zaidi ya wanafamilia 55 kuyakimbia makazi yao katika maeneo ya Yombo Kilakala kwa Bongotonyo, kutokana na Nyumba zao kujaamaji

  Zaidi ya wanafamilia 55 kuyakimbia makazi yao katika maeneo ya Yombo Kilakala kwa Bongotonyo, kutokana na Nyumba zao kujaamaji

Mbunge Mtemvu akiyapima maji kwa kuingia na kujionea

Mbunge Mtemvu akiyapima maji kwa kuingia na kujione

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Yombo Relini Yusufu Marko (kulia) akimwelekeza jambo wakati alipo fika katika maeneo hayo baada ya kuzunguuka maeneo tofauti na  Mbunge Abbas Mtemvu (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO