Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TASWIRA: RAIS WA MSUMBIJI FELIPE JACINTO NYUSI ALIPOLIHUTUBIA BUNGE LA TANZANIA NA KUTEMBELEA MAKAO MAKUU YA CCM DODOMA

Rais Wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi akilihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma huku Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Spika wa Bunge hilo Mh.Anna Makinda wakisikiliza.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi,Waziri Mkuu Mizengo Pinda,Spika wa Bunge la Jamhuri

ya Muungano wa Tanzania na viongozi waandamizi katika serikali ya Msumbiji wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya Rais wa Msumbiji kulihutubia Bunge lao mjini Dodoma.

Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikweteakimtambulisha katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwa Rais wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi wakati Rais huyo wa Msumbiji alipowasili katika makao makuu ya CCM m.Jakayajini Dodoma na kuzungumza na viongozi waandamizi .Kushoto ni Naibu katibu Mkuu wa CCM Bwana Mwigulu Nchemba.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais wa Msumbiji Mhe.Filipe Jacinto Nyusi kwenye Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mjini Dodoma.

Rais wa Msumbiji Mhe.Filipe Jacinto Nyusi akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kuwasili kwenye Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.

Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi akisalimiana na wanachama na wapenzi wa CCM waliojitokeza kumpokea na kumkaribisha Dodoma.

Rais wa Msumbiji Mhe.Filipe Jacinto Nyusi akivishwa skafu na vijana wa Chipukizi wa CCM mkoa wa Dodoma wakati wa mapokezi kwenye Makao Makuu ya Chama.

Baadhi ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ,pamoja na viongozi wengine wa CCM mkoa wa Dodoma wakiimba wakati wa kumkaribisha Rais wa Msumbiji Mheshimiwa Filipe Nyusi kwenye makao makuu ya CCM mjini Dodoma.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoa neno la kumkaribisha
Rais wa Msumbiji na Mwenyekiti wa Chama cha Frelimo Mhe. Filipe Nyusi
kwenye makao makuu ya CCM mjini Dodoma.

Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza kabla ya kumkaribisha Rais wa Msumbiji kuhutubia viongozi mbali mbali wa CCM wakiwemo baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu

Mpigania Ukombozi wa Msumbiji Mzee Aberto Chipande akizungumza kabla ya Rais Filipe Nyusi kuhutubia wana CCM ambapo alielezea namna harakati za kuikomboa nchi yao zilivyoanza, kupangwa na kuratibiwa Kongwa Dodoma na kuanza safari ya kuelekea vitani mwaka 1963 na kusema Dodoma ni nyumbani kwake.

Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu, Viongozi wa CCM mkoa wa Dodoma pamoja na wageni waalikwa wakisikiliza hotuba ya Rais Filipe Nyusi kwenye ukumbi wa NEC mjini Dodoma.

Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi akihutubia kwenye ukumbi wa NEC ,Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.

Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi akijaribu kofia ya CCM ikiwa sehemu ya zawadi alizopewa na CCM.

Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi pamoja na Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete wakiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa halmashauri Kuu ya CCM Taifa mjini Dodoma

Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi akiwaaga wana CCM mara baada ya kuwahutubia ambapo alisisitiza kuwa Frelimo itaendelea kudumisha mshikamano wao na CCM.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO