Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TASWIRA: MAZISHI YA DIWANI VITI MAALUM CCM ARUSHA

sam_2557

Baadhi ya Mdiwani wa jiji la Arusha wakiongozwa na Meya wa jiji hilo Gaudence Lyimo kulia ,wakiwa wamebeba jeneza la Belina Kabuje ambaye alikuwa diwani wa viti maalumu jijini Arusha kuelekea katika katika kanisa la Parokia Mtakatifu ngarenaro jijini hapa jana

SAM_2564(1)

Kushoto ni mtia nia ubunge jimbo la Arusha Filemon Mollel akiwa katika ibada hiyo pamoja na wadau wengine wa CCM

SAM_2575(3)

Mbunge wa zamani wa jimbo la Arusha mjini Felix Mrema akisalimiana na akinana waombolezaji waliofika katika kanisa hilo jana

SAM_2583(2)

Baadhi ya vijana wa jumuiya ya umoja wa vijana wa CCM(Uvccm) wilayani Arusha wakibeba mwili wa marehemu Belina Kabuje ambaye alikuwa diwani wa viti maalumu jijini Arusha kuelekea katika eneo la mazishi eneo la Oljoro nje kidogo ya jiji la Arusha jana
SAM_2566(1)

Mgombea anayetajwa kuwania jimbo la Arusha mjini kupitia CCM, Mustafa Panju ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya Bush Buck Safaris ,pembeni yake akiwa na msaidizi wake  Alhaji Kassim Mamboleo wakiwa katika ibada hiyo jana

---

Mazishi ya diwani wa viti maalumu jijini Arusha,marehemu Belina Kabuje ambaye alifariki hivi karibuni katika hospitali ya rufaa ya KCMC mjini Moshi jana yalitawaliwa na huzuni na hisia mbalimbali mara baada ya familia ya marehemu kuzuiwa isipokee fedha za rambirambi.

Fedha hizo zilizuiwa na meya wa halmashauri ya jiji la Arusha,Gaudence Lyimo wakati akitoa salamu za rambirambi ndani ya kanisa Katoliki Parokia ya Roho Mtakatifu Ngarenaro wakati mwili wa marehemu ulipofikishwa kwa ajili ya ibada.

Akizungumza wakati akitoa salamu hizo bila kutaja kiasi chake  meya huyo alisema kuwa fedha zote zilizokusanywa kama rambirambi ya marehemu hazitakabidhiwa mbele ya familia yake hadi pale utaratibu wa kufungua akiba utakapokamilika.

Alisema kuwa lengo la kuweka utaratibu huo ni kuepusha matumizi mabaya ya fedha hizo kutumika hovyo huku akisisitiza ya kwamba marehemu enzi za uhai wake alikuwa mtu mwenye hofu na mashaka .

“Marehemu enzi za uhai wake alikuwa na hofu sana kuna  mambo mengine yalikuwa ni siri kwa familia lakini alilazimika kutushirkisha sisi madiwani”alisema Lyimo

Hatahivyo,katika hali isiyo ya kawaida baadhi ya waombolezaji waliohudhuria kanisa hapo walijikuta wakipiga makofi kushangilia hotuba ya meya huyo pale alipotamka ya kwamba mali za marehemu huyo kamwe hazitaguswa na mtu yoyote kwa kuwa kuna wosia umeachwa na marehemu.

Naye,mwenyekiti wa jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa CCM(UWT) mkoani Arusha,Flora Zelothe aligusa hisia za watu  kanisani hapo mara baada ya kutamka kwamba marehemu aliacha wajukuu watatu ambao alikuwa akiwahudumia na kudai kimsingi wanapaswa kutambuliwa na familia.

Hatahivyo,paroko wa kanisa hilo,Anchi Mpota akiendesha ibada ya kumuombea marehemu huyo aliwataka watu kuondoa tofauti zao za kidini,kikabila na kisiasa kwa madai kwamba zitawagawa.

“Kwa hali ilivyo sasa amani tuliyonayo tusiichezee tuondoe tofauti zetu za kidini,kisiasa na kikabila kama tukiziendekeza basi zitatugawa”alisema paroko huyo

CHANZO: JAMII BLOG (PAMELA MOLLEL)

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO