Mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa akiwapungia mikono wafuasi wake waliofika katika uwanja wa msikiti mkuu katika hafla ya harambee ya ujenzi wa msikiti wa Patandi ambapo jumla ya kiasi cha zaidi ya sh,200 milioni zilipatikana katika harambee hiyo(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
Umati mkubwa wa wananchi wa Arusha wakiwa wanampungia mkono mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa akiwapungia mikono wafuasi wake waliofika katika uwanja wa msikiti mkuu katika hafla ya harambee ya ujenzi wa msikiti wa Patandi ambapo jumla ya kiasi cha zaidi ya sh,200 milioni zilipatikana katika harambee
Mbunge wa jimbo la Monduli,Edward Lowasa akiwa sheikh mkuu wa Bakwata mkoani Arusha,Shaaban Juma wakifurahia jambo katika hafla ya harambe ya ujenzi wa msikiti wa Patandi iliyofanyika jana katika uwanja wa msikiti mkuu wa mkoa Arusha,jumla ya kiasi cha zaidi ya sh,200 milioni zilipatikana.
Mkurugenzi wa kituo cha Redio 5 Arusha Francis Robart akiwa anawasilisha jumla ya fedha zilizopatikana katika harembee hiyo kwa Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli,Edward Lowasa.
Mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa akiwapungia mikono wafuasi wake waliofika katika uwanja wa msikiti mkuu katika hafla ya harambee ya ujenzi wa msikiti wa Patandi ambapo jumla ya kiasi cha zaidi ya sh,200 milioni zilipatikana katika harambee
Mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa akiwa anasalimiana na baadhi ya wadau waliokuja kumuunga mkono katika uwanja wa msikiti mkuu katika hafla ya harambee ya ujenzi wa msikiti wa Patandi ambapo jumla ya kiasi cha zaidi ya sh,200 milioni zilipatikana katika harambee
Taswira ya picha wakati mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa akiwa anaondoka katika uwanja wa msikiti mkubwa jijini Arusha
Msafara wa pikipiki
Mgombea anayetajwa kuwania jimbo la Arusha mjini kupitia CCM, Mustafa Panju ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya Bush Buck Safaris akiwa anasalimiana na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa baada ya kumkabidhi shilingi Milioni sita kwaajili ya ujenzi wa msikiti Patandi.
Diwani Mathias Manga akiwa anawasilisha mchango wa rafiki yake wa karibu Husein Gonga wa shilingi Milion saba.
Mkurugenzi wa Redio 5 Arusha Francis Robart kulia wakiwa wanapiga hesabu ya jumla ya fedha zilizopatikana
Kada maarufu wa chama cha CCM,Violet Mfuko katikati akiwa na diwani viti maalum Vick Mollel wakiwa wanamshangilia mgeni rasmi mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa katika hafla ya harambee ya ujenzi wa msikiti wa Patandi ambapo jumla ya kiasi cha zaidi ya sh,200 milioni zilipatikana katika harambee hiyo
Kushoto ni mtia nia jimbo la Arumeru mashariki Solom Sioi pamoja na mkuu wa Wilaya ya Arumeru Husna Mwilima wakifatilia jambo katika harambee hiyo
Mbunge wa Kigoma mjini Peter Serukamba akiwasilisha mchango wake
Wananchi wakiwa wanamsikiliza Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa
**************
KUTANGAZA NIA YA URAIS MEI 24
Waziri mkuu wa zamani na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa anatarajia kutangaza nia ya kuwania nafasi ya Urais kupitia CCM mnamo Mei 24 mwaka huu katika uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid uliopo jijini Arusha.
Lowasa,alitoa kauli hiyo leo katika harambee ya kuchangia ujenzi wa msikiti wa Patandi ambapo alifanikisha kuchangisha jumla ya zaidi ya kiasi cha sh,200 milioni ambapo watu mbalimbali walimuunga mkono katika harambee hiyo.
Akizungumza katika hafla hiyo leo kwa mafumbo Lowasa alisema kuwa mnamo Mei 24 mwaka huu anataraji kusema neno ambalo atahitaji wananchi wamuunge mkono siku hiyo.
"Niseme neno nisiseme,tarehe 24 mwezi huu katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid siku hiyo nitasema neno ambalo nitahitaji mniunge mkono ambalo nitahitaji mniunge mkono "alisema Lowasa
Lowasa kwa kujiamini aliwaomba kila mkazi wa Arusha siku hiyo kutoka na kuja uwanja huo na kumuunga mkono katika safari yake ya matumaini.
"Ukiulizwa unaenda wapi sema unakuja kuniunga mkono katika safari yangu ya matumaini"alisisitiza Lowasa
Hatahivyo,Lowasa aliipongeza kamati ya amani ya mkoa wa Arusha inayoundwa chini ya Askofu wa kanisa katoliki la jimbo kuu mkoani Arusha,Josephat lobullu kusimamia amani ya mkoa huo.
Aliipongeza kamati hiyo na kusema kuwa amani ya mkoa wa Arusha ni muhimu kuliko jambo lolote kwa kuwa Arusha ni mji ambo ni chanzo cha utalii duniani.
"Tuendelee kuheshimiana bila kujali misingi ya dini,kabila au rangi lakini niipongeze kamati ya amani ya hapa Arusha kwa kuwa Arusha ni mji wa kitalii bila amani hakuna utalii Arusha"alisema Lowasa na kuibua shangwe.
Chanzo:Michuziblog
0 maoni:
Post a Comment