Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha wakiwa kwenye mkutano ambao walitoa tamko la kupinga uongozi wa chama wilaya kuwaburuza kwenye mchakato wa ubunge wilayani humo.
Arusha.Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) wilaya ya Monduli zaidi ya 600 wamewatuhumu viongozi wa chama hicho kwa kuwaburuza katika maamuzi na kuwaamulia nani atakua mbunge wa Jimbo hilo baada ya Mbunge wa sasa,Edward Lowassa kutajwa kutogombea nafasi hiyo.
Wana CCM hao kutoka Kata zote 20 walidai kumekuwepo na ukiukwaji wa makusudi wa kanuni za chama unaongozwa na Katibu wa CCM wilaya,Elisante Kimaro kufanya ziara za kichama na mmoja wa waliotajwa kugombea ubunge jimbo hilo na kumtambulisha kinyume na kanuni za chama hatua iliyozusha mgogoro na kuhatarisha uhai wa chama.
Katika barua yao kwa Katibu wa CCM mkoa,Alphonce Kinamhala inawataja moja kwa moja Mjumbe wa kamati ya Siasa ya mkoa,Paulo Kiteleki ambaye ni Katibu Tarafa ya Kisongo,Mjumbe wa Kamati ya Siasa na maadili wa wilaya ,Kalaine Lowassa,Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake(UWT)wilaya,Einoti Leringa na Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Monduli,Edward Sapunyu.
Wengine wanaotuhumiwa kukiweka chama rehani kwa maslahi yao ni Mjumbe wa Kamati ya siasa ya wilaya ambaye pia ni diwani wa Kata ya Monduli Juu,Bariki Sumuni na Katibu wa Hamasa wa Umoja wa vijana(UvCCM)Kimani Ndiarakombe.
“Tunaomba viongozi wetu wakumbuke ya kuwa kuwepo CCM ni kuwepo kwa wanachama ambao haki zao zinaheshimiwa na kupewa demokrasia ndani ya chama chao na sio viongozi wa ngazi husika wanaamuakwa maslahi yao kukiuka taratibu za chama kwasababu wamepewa dhamana ya kuwa viongozi.”ilisema sehemu ya barua hiyo
Hata hivyo Katibu wa CCM wilaya ya Arusha ,Elisante Kimaro alikanusha taarifa hizo na kudai hazina msingi wowote bali kinachofanyika ni ziara ya kawaida ya kuwashukuru wananchi kutokana na ushindi mkubwa walioupata kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka jana ambapo Mbunge wa Viti Maalum,Namelok Sokoine ni Mjumbe ambaye ametoa mchango mkubwa kwa wanawake na vijana.
Mwakilishi wa Kata ya Lorkisale,Lembrisi Klamian na Parmelo Ngoyo kutoka Kata ya Sepeko walisema zama za kuburuzwa zimepitwa kila jambo linapaswa kufanyika kwa ushirikishwaji na sio kuwapandikiza wagombea wao bila ridhaa za wanachama.
Wanachama hao wamesema iwapo malalamiko yao hayatashughulikiwa ipasavyo na kwa wakati kwasababu wanaolalamikiwa ni wajumbe wa kamati za maamuzi ngazi ya wilaya na mkoa watalazimika kutafuta njia mbadala ya kufikisha malalamiko yao kwa uongozi wa ngazi ya taifa.
Wanachama Teshi Oloing’ola kutoka Kata ya Lepurko na Osidai Nadongala wa Kata ya Mbwakiri walisema kinachowasikitisha ni kuwa wajumbe wa kamati ya siasa na kamati ya maadili wilaya kwenye kampeni za kumnadi mgombea anayenadiwa na msimamia taratibu za chama ambaye ni Katibu wa wilaya.
Hata hivyo walidai viongozi hao wa wilaya kutumiwa na mmoja wa viongozi wakubwa wilayani humo bila kutaja jin
KWA HISANI YA RWEYEMAMU INFO BLOG
0 maoni:
Post a Comment