Katibu wa BAWACHA Taifa Mh Grace Tendega akihutubia katika Mkutano Mkuu wa BAWACHA Jimbo la Arusha Mjini ambapo alikuwa mgeni rasmi. Mh Tendega amewaambia wanawake wenzake kuwa mwaka huu ni mwaka wa mwisho kwa chama chake CHADEMA kuwa wapinzani kwasababu wamejipanga kuhakikisha wanashinda katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba baadae mwaka huu na kukabidhiwa dola kwa mara ya kwanza.
Katibu huyo ambaye alizindua vazi rasmi la BAWACHA Arusha Mjini katika mkutano huo, aliwaeleza wanawake wenzake wa CHADEMA kuwa wana kila sababu ya kushinda uchaguzi huu kwasababu watanzania wako tayari kwa mabadiliko na kwamba kinachohitajika ni kuwahamasisha zaidi.
Mh Tendega aliwataka wanawake hao kuwashawishi wanawake wenzao wanaoweza kuwa viongozi na wanakubalika na jamii washiriki kuogombea nafasi mbali mbali za uongozi katika uchaguzi huu. Akisisitiza zaidi aliwatahadharisha kuwa ushindi huo haotokuja tu bila kujiandikisha na hivyo akawataka kuhamsisha wananchi kujinadikasha kwa wingi iwezekanavyo pindi zoezi la uandikishaji litakapowafikia ijapokuwa alidai NEC inabahatisha tarehe zake.
Aidha, alitumia nafasi hiyo aliyopata kuhutubia kuwashukuru watu wa Arusha ambao alidai walisaidia kwa kiasi kikubwa katika kampenzi za uchaguzi mdogo wa Kalenga mwaka jana na kuwasihi wasichoke kuendelea kuhamasisha na maeneo mengine.
Akimzungumzia Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema, Mh Tendega alidai kuwa wao mikoani wanamtambua kama mbunge wa Taifa na sio wa Arusha pekee.
Wamama wa BAWACHA wakiserebuka kumuunga mkono mwanamama mwenzao aliyetambulisha nyimbo zake
Mratibu wa BAWACHA Mkoa wa Arusha Mh Cecy Ndossi
Viongozi wa BAWACHA Jimbo la Arusha Mjini
Mke wa Mbunge wa Arusha Mjini Bi Neema Lema akifuatilia yanayojiri mkutanoni
Wamama wakiwa wamependeza na mavazi yao maridadi yenye nakshinakshi ya rangi za Chadema
0 maoni:
Post a Comment