Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli Mh. Edward Lowassa amechangisha jumla ya shilingi millioni 234 katika Harambee ya kuchangia ujenzi wa Msikiti wa Patandi uliopo wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha ambayo awali ilitangazwa kuwa mgeni Rasmi katika Harambee hiyo angekuwa Mheshimiwa Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyepata udhuru na badala yaek ndio Edward Lowassa akamuwakilisha. Fedha hizo ni pamoja na fedha taslimu na ahadi.
Katika Harambee hiyo, Mbunge wa Arusha Mjini Mh. Godlbess Lema kupitia tiketi ya CHADEMA amechangia jumla ya shilingi milioni 1 kusaidia ujenzi wa msikiti huo.
Msikiti wa Patandi upo katika eneo wanalokaa wananchi wenye imani mbalimbali na waumini wanaoutumia msikiti huo, na wamekuwa wakijitoa kwa namna nyingi katika kusaidia kujenga mshikamano baina ya jamii zinazowazunguka bila kuwa na vikwazo na pia wamekuwa wakishiriki katika kuwasaidia watoto yatima na wengine wenye uhitaji katika kukabiliana na maisha yao.
Mh Lowassa akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Msikiti wa Patandi
0 maoni:
Post a Comment