Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MATUKIO ZAIDI: GRACE TENGEGA WA BAWACHA TAIFA NA MKUTANO WA HADHARA SOKO KUU NA UZINDUZI WA TAWI JIJINI ARUSHA

DSC_0128

Katibu wa BAWACHA Taifa Bi Grace Tendega akihutubia wakazi wa Arusha Mjini waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara uliondaliwa na BAWACHA Wilaya ya Arusha Mjini na kufanyika katika eneo la Soko Kuu Arusha, Kata ya Kati. Kabla ya hapo Mh Tendega alikuwa mgeni rasmi kwenye Mkutano Mkuu wa BAraza hilo kwa Wilaya ya Arusha Mjini ambapo viongozi wa baraza hilo kwa Kata zote za Arusha Mjini pamoja na wenyeviti wa Serikali za Mitaa wanawake watokanao na CHADEMA.

Katika mkutano wa Soko Kuu, Tendega aliwahimiza wakazi wa Arusha kujitokeza kwa wingi na kuhamasishana kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili waweze kushiriki uchaguzi mkuu baadae mwaka huu na kutimiza kile wanachoamini kuwa ni kushinda uchaguzi huo na kukamata dola.

DSC_0162

DSC_0155

Akisisitiza jambo

DSC_0167

Grace Tendega akiagana na wana Arusha mkutanoni hapo kwa ishara ya kukunja ngumi na kuitikia salamu ya “people’s…power”

DSC_0183

Katibu wa CHADEMA Kata ya Kati ulipofanyika mkutano huo Bw Hassan Noor akipozi kwa picha na viongozi wanamama mara baada ya mkutano

DSC_0141

Meza kuu mkutanoni

DSC_0189

Msafara wa Katibu wa BAWACHA Taifa Mh grace Tendega akiongozwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Arusha Amani Golugwa wakiwasili katika eneo la stand ya ‘mabasi luxury’ Levolosi ambapo kulikuwa na zoezi la uzinduzi wa tawi la CHADEMA na yeye ndiye aliyepewa heshima ya kufanya uzinduzi huo rasmi.

DSC_0196

Maandalizi ya uzinduzi wa tawi kwa kupandisha bendera. Wajumbe wametulia kusikiliza maelekezo

DSC_0206

Mh Grace tendega akipandisha bendera kumaanisha uzinduzi rasmi wa tawi

DSC_0210

Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Arusha Amani Golugwa akitoa neno kwa wanatawi na mashuhuda wengine wa tukio hilo la uzinduzi

DSC_0212

Grace Tendega akizungumza mara baada ya uzinduzi rasmi

DSC_0220

Mwananchi akiwa amemganda Mh tendega wakati akiondoka

DSC_0011Munge wa Arusha Mjini na Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA Mh Godbless Lem pamoja na Mweyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Arusha ambaye pia ni Mratibu wa Kanda ya Kaskazini ya chama hicho Mh Amani Golugwa wakiwa wametandwa na vitambaa ambavyo vilizinduliwa maaluamu kwa kushonea vazi la wanawake wa BAWACHA Arusha. Wengine katika picha ni Katibu BAWACHA Taifa Bi Grace Tendega na Mratibu wa BAWACHA Mkoa wa Arusha Bi Cecilia Ndossi

DSC_0173

Bosi mzito wa Blog hii SeriaJr akipozi na timu ya viongozi wa BAWACHA akiwemo Katibu Mkuu Grace Tendega anyecheka katikati yao

DSC_0143

Wanahabari wakipozi kwa snaposhot ya Arusha255. Kulia ni Grace Macha wa Tanzania Daima na Makabayo ambaye ni Afisa wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO