Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Chadema: JK aache “safari za ovyo”

KAMATI Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), imeazimia na kulaani tabia ya Rais Jakaya Kikwete kusafiri ovyo nje ya nchi wakati taifa lipo katika kipindi kigumu na matatizo makubwa ambayo yanahitaji uongozi thabiti.Kamati Kuu ilikutana kwa siku mbili kati ya tarehe 3 hadi 5 Mei mwaka huu, na kuitaka pia serikali kuchukua hatua za dharura kunusuru shilingi kwani athari zake ni kubwa sana kiuchumi na kijamii na kwamba zitasababisha mfumuko wa bei.


Akisoma maazimio hayo leo kwa waandishi wa habari katika Makao Makuu ya Chadema yaliyopo mtaa wa Ufipa Kinondoni, Katibu Mkuu wake, Dk. Willibrod Slaa, amesema kamati kuu vile vile ilipokea na kujadili hali halisi ya sekta ya usafirishaji nchini.


Amesema kuwa, wamebaini udhaifu mkubwa ambao upo ndani ya sekta hiyo kutokana na usimamizi dhaifu wa watu ambao walipewa dhamana kuanzia Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta ambaye ameshindwa kabisa.


“Hali hiyo inasababisha sekta hiyo kukosa mwelekeo na hivyo kuleta madhara mengi kwa wananchi kutokana na ajali za kila siku kuanzia vyombo vya majini na barabarani. Kamati kuu imebaini kutokana na mgomo wa madereva wananchi wameathirika kisaikolojia na kiuchumi,”amesema.
Kwa mujibu wa Dk. Slaa, Kamati kuu, imeazimia kuunga mkono madai ya madereva kwani ni halali na hivyo ni lazima serikali iyatekeleze madai yao yote ya muda mrefu. Amesema “kuendelea kuyapuuza ni kukubali kuendelea kuhatarisha maisha ya abiria.”

Kuhusu uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu, Dk. Slaa amesema kamati kuu imepokea taarifa ya kina namna ambavyo hadi sasa maandalizi ya msingi kisheria hayajafanyika. Ametaja kuwa ni mandalizi ya vifaa, fedha, kutangaza majimbo na kata mpya, kutangaza vituo na kusuasua kwa uandikishaji wapiga kura.
“Katika jambo hili, kamati kuu imeazimia kuwa uchaguzi huo lazima ufanyike Oktoba kwa mujibu wa Katiba na serikali ya CCM isijiandae kutumia kisingizio chochote kuahirisha kwa sababu uchaguzi sio jambo la dharura, bali lilijulikana miaka mitano iliyopita,” amefafanua

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO