Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

ACT yaomba kujiunga UKAWA

mghi

Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo Anna Mgwira (pichani) amesema chama hicho hakina matatizo na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na hata sasa kinasubiri majibu ya barua yao waliyoituma kwa umoja huo kuomba kuunganishwa.

Mgwira alitoa kauli hiyo wakati chama hicho kilipofanya ziara ya kutembelea hospitali ya mkoa ya Mt Meru kugawa zawadi mbalimbali katika wodi ya kinamama ikiwa ni njia ya kuadhimisha mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake.

Alisema ACT-Wazalendo wanaunga mkono muungano wowote wa vyama vya upinzani nchini ulio halali.

“Hatuna matatizo na Ukawa tunaunga mkono muungano wowote wa upinzani ulio halali,” alisema kiongozi huyo

Alisema tangu waandike barua ya kuomba mwongozo wa namna ya kujiunga na Ukawa, bado hawajapata mrejesho.

“Tunatamani kuunganisha nguvu katika siasa za vyama vya upinzani na sasa tunasubiri majibu ya barua yetu ya kuomba kuingia Ukawa,” .

Alisema kuwa chama hicho kimepokewa vizuri na wananchi wa mikoa mbalimbali nchini na katika ziara ya awamu ya kwanza walifanikiwa kuingiza jumla ya wanachama wapya 700.

Tumepokewa vizuri mikoani tumefanikiwa kuingiza wanachama wapya na hoja ya umoja na uzalendo watu wameipokea vizuri,” Mgwira.

Akipokea misaada katika hospitali hiyo Muuguzi Mfawidhi, Sifael Masawe alisema kwamba misaada hiyo itasaidia kupunguza shida za wagonjwa.

CHANZO: MWANANCHI

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO