Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Lema Asaini Mkataba wa Ujenzi wa Hospitali ya Mama na Mtoto!

Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema kupitia Arusha Development Fund (ArDF) amesaini makubaliano na wafadhili kufanikisha ujenzi wa hospitali ya Mama na Mtoto Jijini Arusha wenye thamani ya US$ Mil 3.2

Makabidhiano hayo yamefanyika eneo la Burka katika kiwanja ambacho Lema alikabidhiwa na Mawalla Advoctes mapema leo asubuhi. Jiji la Arusha leo liko kwenye furaha kubwa baada ya utiaji saini wa mbunge wa Arusha mjini mhe. Godbless Lema na kampuni ya Maternity Leave Africa itakayo simamia ujenzi wa hospitali hiyo ya Mama na Mtoto. Akiongea na wananchi wa Arusha waliojitokeza katika zoezi hilo lema alisema kwake ni siku mhimu sana ila ana hudhuni moj tu kuwa mtu aliempa kiwanja ambacho kwasasa kiana thamani ya takribani dola laki nne (US$ 400,000) alisema jambo hili anataka limpe heshima kwaajili ya UTU na siyo kwa kampeni zitakazo anza karibuni, na kati ya vitu ambavyo nitajivunia ni kumbukumbu ya maisha ya binadamu ambayo mimi ni kiongozi. Alisema ni heshima kubwa kutimiza ndoto hiyo aliyoianza miaka mitano iliyopita kutokana na kero alizozishuhudia kwenye hospitali ya mkoa wa Arusha (Mt Meru Hospital) maisha ya mama na watoto yanatuhitaji wote, hatutafuti umarufu kisiasa kwani alipofikilia wazo hili wakati huo siyo Mbunge hakujua hata ataanzia wapi na mpaka wakati huu hajuai nini kinaendelea kweli Mungu anatenda miujiza. Aliwaambia Shirika la Maternity Leave Africa siyo tu kuwa anawapa eneo bali yuko tayari kusaidia kwa vyovyote vile na kwa kuanza ametoa matofari yasiyopungua 5,000.. pamoja na kusaini ujenzi huo wiki ijayo atakabidhi Ambulance kwa hospitali ya Mt Meru. Akitoa shukrani zake Mwenyekiti wa ArDF Elifuraha alisema Hospital hii haitakuwa ya mama na watoto wasio na uwezo tu bali ya Mama na Watoto wa Tanzania wote pia aliwashukuru madaktari bingwa waliotoa ushauri juu ya hopitali hii na kwa Godbless lema kwa maono yake na kumpa pole mke wa Mbunge (Neema) kwa kuhusishwa na mashetani kuwa eti amemilikishwa kiwanja hicho. Mwenyekiti wa Arusha Development Fund (ArDF) Elifura, Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema na Dr Adrew Wakisaini mkataba wa ujenzi wa Hospitali ya Mama na Mtoto huku wakishuhudiwa na viongozi mbalimbali wa kisiasa na kiserikali.

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO