Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Waziri wa Ulinzi Korea Kaskazini Auawa Kwa bunduki ya Kutungulia Ndege Akituhumiwa Kusinzia Kwenye Mkutano wa Rais

Hyon Yong-Chol aliyeuawa kwa kusinzia wakati wa hafla ya kijeshi.

WAZIRI wa Ulinzi wa Korea ya Kaskazini, Hyon Yong-Chol, ameuawa kwa kupigwa na bunduki ya kutungulia ndege aina ya ZPU-4 kwa kusinzia kwenye hafla ya kijeshi. Waziri huyo aliuawa kutokana na amri ya kiongozi wa nchi hiyo, Kim Jong-Un.

Bunduki ya kutungulia ndege aina ya ZPU-4  iliyotumika kumuua Hyon.

Sababu nyingine iliyomfanya waziri huyo aliyekuwa na umri wa miaka 66 na aliyekuwa kiongozi wa jeshi la nchi hiyo tangu mwaka 2012 auawe, ni kutoa kauli za kumpinga kiongozi wa nchi hiyo, Kim Jong-Un katika matukio kadhaa.

Hyon aliuawa mbele ya mamia ya maofisa wa serikali na jeshi katika kambi moja mjini Pyongyang tarehe 30 Aprili mwaka huu ambapo aliyemuua alisimama umbali wa futi 100 tu akitumia bunduki hiyo ambayo inaweza kufika umbali wa futi 26,000.

Hyon (kulia) alichaguliwa mwaka 2012 kuwa Waziri wa Ulinzi wa Korea ya Kaskazini.

Uchunguzi umeonyesha kwamba watu wengi waliuawa kwa kutumia njia hiyo ya kikatili katika kambi hiyo mwezi Oktoba mwaka jana.

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO