Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

UVCCM MBEYA WAANZA KAZI

  

Mwenyekiti  wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi CCM (UVCCM) Mkoa wa Mbeya , Amani Kajuna, akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi katika eneo la Sogea Tunduma wilayani mombaMei 4 mwaka huu.

Wanachama wa ccm na wananchi wakimsikiliza Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Uvccm Mkoa wa mbeya Amani Kajuna katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Sogea Tunduma Wilayani Momba.

 

Mwenyekiti Kajuna akizungumza na wananchi na wanachama wa CCM katika mkutano huo uliofanyika katika eneo la Sogea Tunduma Momba Mkoani Mbeya Mei 4 mwaka huu.

Mjumbe wa kamati ya siasa Mkoa Hasani Nyalile akizungumza katika mkutano huo.

Katibu wa UVCCM Mkoa wa Mbeya Adia Mamu akizungumza na wanachama wa CCM na wananchi walifika katika mkutano huo eneo la sogea Tunduma Momba Mkoani Mbeya Mei 4 mwaka huu.

Msanii wa Nyimbo za Asili Awilo akitumbuiza katika mkutano huo.

Mkutano ukiendelea

Kikundi cha sanaa cha Makirikiri kikitoa burudani katika Mkutano huo ulioandaliwa na Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Mbeya chini ya Mwenyekiti Amani Kajuna Mei4 mwaka huu.Picha Emanuel Madafa

Umoja wa vijana wa CCM mkoa wa Mbeya(uvccm) umetoa siku tatu kwa Mbunge wa jimbo la momba David Sillinde kuziwasilisha fedha za mfuko wa jimbo kiasi cha shilingi milioni 46 anazodaiwa kuzihafadhi kwa ajili ya kumsaidia kwenye kampeni yake ili zifanyie maendeleo

Akizungumzia hilo, mwenyekiti wa umoja huo, amani kajuna, katika mkutano wa wananchi katika eneo la sogea tunduma wilayani momba, amesema sillinde anapaswa kuziwasilisha fedha hizo kwenye mamlaka husika ili zifanyie shughuli za maendeleo.

''Kiasi hiki cha fedha cha shilingi milioni 46 kinatokana na kodi za wananchi na ni kwa ajili ya kutekeleza shughuli za maendeleo hivyo kitendo cha mbunge kuzikumbatia ni ukiukwaji wa sheria, umoja wa vijana tunamtaka kuziwasilisha fedha hizo ndani ya siku tatu,"

Aidha, mwenyekiti huyo, amechangia mifuko 10 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa kisima cha maji katika eneo la sogea mjini tunduma.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO