Baraza la Wanawake CHADEMA Wilaya ya Arusha Mjini hii leo limefanya Mkutano Mkuu wa Baraza hilo Wilaya katika Ukumbi wa Twiga katika Hoteli ya New Safari ambapo Katibu Mkuu Taifa Mh Grace Tendega amealikwa kama mgeni rasmi. Mkutano huo umewakutanisha kina mama viongozi wa CHADEMA wasiopungua 300 kutoka Kata mbalimbali za Jimbo hilo. Viongozi wengine walioshiriki ni pamoja na Mjumbe wa Kamati Kuu Taifa Dk Heri Macha.
Viongozi wanaume wa CHADEMA Arusha walialikwa pia akiwemo mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema na Mwenyekiti wa CHADEMA wa Mkoa wa Arusha Mh Amani Golugwa pamoja na viongozi wengine wa Wilaya.
Mkutano huu Mkuu wa BAWACHA utafuatiwa na Mkutano Mkubwa wa hadhara utakaofanyika eneo la Soko Kuu Kata ya Kati, Jijini hapa. Slogan yao ikiwa “Wanawake – Chimbuko la Maendeleo”
Mjumbe wa Kamati Kuu Taifa ambaye ni mlemavu wa macho, Dk Heri Macha akizungumza kuwatia moyo kina mama wenzake waliohudhuria Mkutano Mkuu wa BAWAHA Arusha Mjini uliofanyika katika Hoteli ya New Safari; hasa ambao wanadhani ulemvu ni kizuizi cha wao kushiriki siasa kama wanajamii wengine. Wanaomtazama ni Katibu wa BAWACHA Taifa Mh Grace Tendega na Mwenyekiti wa BAWACHA Mkoa wa Arusha Mh Cecy Ndosi
Sehemu ya meza kuu; kutoka kushoto ni Katibu Mkuu BAWACHA Taifa Bi Grace Tendega, Mwenyekiti wa BAWACHA Mkoa wa Arusha Bi Cecy Ndossi, Mjumbe wa Kamati Kuu Taifa CHADEMA Dk acha.
Katibu wa BAWACHA Wilaya ya Arusha Mjini ambao ndio waandaaji wa Mkutano huu, ambaye pia ni Diwani wa Viti Maalumu Kata ya Lemara CHADEMA Mh Viola Lazaro Likindikoki akihutubia mkutano huo kwa kusoma ripoti ya BAWACHA Arusha Mjini kabla ya kuikabidhi kwa mgeni rasmi.
Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA) akizungumza kuhutubia kinamama wa BAWACHA Arusha Mjini ambapo aliwapongeza kina mama kwa mafanikio makubwa waliyofikia kwa umoja wao.
Mh Lema aliutaarifu mkutano huo kuwa kwa taarifa za kitafiti ilizo nazo CHADEMA, hakuna namna CCM inaweza kuendelea kuwa madarakani na kwamba kwa upande wa ubunge tu wana majimbo takribani 147 ambayo wana uhakika wa kushinda bila shaka kwa upande wa CHADEMA na mengine ambayo hakutaja idadi yake yakiachwa kwa upande wa washiriki wenza wa UKAWA.
Akisisitiza zaidi Mh Lema aliwataka kina mama ambao alidai ndio wapiga kura muhimu ambao wamekuwa mtaji wa chma tawala kwa miaka mingi huku wao wakiwa ndio wanaoteseka na madhila mbalimbali ya nchi, kwamba mbali na ishara zote kuwa chama tawala kitang’oka lakini haitakuwa rahisi bila kushinda majimbo mengi, jambo alilodai litafanikiwa kwa kujiandikisha kwa wingi.
Lema alienda mbali zaidi akigusia zoezi la uandikishaji wapiga kura na kueleza kuwa kuna dalili zote kuwa chama tawala kinajaribu kutumia hila na nguvu za serikali kuahirisha uchaguzi wa mwaka huu katika kile alichodai ni mbinu za kujiokoa na uwezekano wa kushindwa katika uchaguzi huo. Akifafanua zaidi, aliwaomba kina mama hao kuwa tayari muda wowote kukataa jaribio lolote la kuahirisha uchaguzi huo hata kama ni kwa maandamano.
Huku akishangiliwa na kina mama viongozi waliohudhuria, Mh Lema alisema kwa kuiamini kuwa yeye yupo tayari kwa Uchaguzi hata kesho na kudai kushangaa wapinzania wake kuhangaika nae ilhali wao wakienda Kata fulani Jimboni kwake yeye anaondoka kwenda kuhamasisha maeneo mengine ya nchi.
Kina mama wakishangweeka
Viongozi wa BAWACHA Arusha Mjini; Mwenyekiti Happy Charles na Katibu Viola Likindikoki wakifuatilia mkutano kwa utulivu
Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Arusha ambaye pia ni Katibu ya Kanda ya Kaskazini Mh Amani Golugwa akimkabidhi Mwenyekiti wa BAWACHA Mkoa wa Arusha Mh Cecy Ndossi
Kikundi cha sanaa na ngoma za utamaduni cha AYOTA kutoka Jijini Arusha kikiburudisha ukumbinu hapo. Kutoka ni Sylvia, Joanes, Benson na Aneth
Viongozi wa CHADEMA Wilaya na Mkoa wakishiriki kucheza ngoma. Kushoto ni Mwenyekiti wa Wilaya ya Arusha Mjini Mh Derick Magoma akifuatiwa na Mwenyekiti wa Mkoa Mh Amani Golugwa
Ngoma imenoga
Meza kuu, kutoka kushoto Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema, Mwenyekiti wa Mkoa Amani Golugwa, Katibu BAWACHA Taifa Mh Grace Tendega, Mwenyekiti wa BAWACHA Mkoa wa Arusha Mjini Mh Cecy Ndossi ambaye ametangaza nia ya kuwania Ubunge Jimbo la Monduli na Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA Taifa Dk Macha.
Msafara wa Mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha CHADEMA akiwasili ukumbini kwa kupokelewa na Mwenyekiti wa BAWACHA WIlaya Mh Happy Charles
Waajumbe waliohudhuria
Viongozi wa CHADEMA Wilaya ya Arusha Mjini kama wageni waalikwa; kutoka kulia Katibu Mwenezi Wilaya Mh Gabriel Kivuyo, Mwenyekiti Derick Magoma na Katibu Wilaya Lewis Kopwe.
Heshima kwa wimbo wa Taifa
Safu ya Viongozi wa BAWACHA WIlaya ya Arusha Mjini. Kutoka kushoto ni Mweka Hazina Mama Thea, Mwenezi Mama Sabina, Katibu Diwani Happy Lazaro na Mwenyekiti Mama Happy Charles
Katibu wa BAWACHA Wilaya ambaye pia ni Diwani wa Viti Maalumu Mh Happy Lazaro akiserebuka
Katibu wa Baraza la Wazee CHADEMA Arusha Mjini Bibi Theresa Minja akifuatilia kwa makini hotuba mbalimbali
Mjumbe wa Kamati Kuu ambaye ni mlemavu wa macho Dk Macha akiongozwa na Mwenyekiti wa Mkoa BAWACHA Mh Cecy Ndossi
0 maoni:
Post a Comment