Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA ambaye pia ni mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Mh Tundu Lissu akihutubia umati mkubwa wa wakazi wa Jiji la Arusha katika viwanja vya Shule ya Msingi Ngarenaro katika mkutano uliokuwa katika sura ya UKAWA kwa kuwashirikisha NCCR Mageuzi.
Mkutano huo nusura uathiriwe na mvua kubwa iliyonyesha wakati Mbunge wa Kigoma Kusini Mh David Kafulila akihutubia lakini mapenzi ya wafuasi wa CHADEMA kwa chama na viongozi wao yaliwafanya wavumilie kunyeshewa mpaka mwisho. Viongozi walikataa kukingwa na mvua hiyo na kujikuta wote wakilowa mwili mzima kama wananchi wengine.
Katika hotuba yake, Mh Lissu aliwaeleza wakazi wa Arusha kitendo cha Serikali ya CCM kukorofishana na karibu kila kundi la jamii kwa kutaja wafanyabiashara, walimu, madaktari, madereva, wafanyakazi n.k ni ishara kuwa chama hicho kimechokwa na kinaweza kuondoka madarakani katika Uchaguzi wa mwaka huu ambao alisisitiza ni lazima ufanyike mwaka huu.
Msafara wa Viongozi wa UKAWA. Kutoka Kushoto Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema, Mbunge wa Singida Mashariki Mh Tundu Lissu, Mbunge wa Kigoma Kusini Mh David Kafulila, Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa Patrobas Katambi na mwanausalama wa CHADEMA
Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR Mageuzi), Mh David Kafulila ambaye kwa siku za karibuni amejizolea sifa lukuki kwa kuweza kuanzisha sakata la ESCROW na kulisimamia mpaka mwisho bila kuhofia vitisho mbalimbali. Katika mkutano huo Kafulila aliwashukuru wakazi wa Arusha kwa mapokezi mazuri na kusisitiza kuwa anajisikia furaha sana kuhutubia umati mkubwa Jijini hapa ambapo ni mji wa kihistoria katika harakati nyingi za kisiasa nchini. Kafulila aliwataka wakazi wa Arusha kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura na kwamba wawe na imani kupitia UKAWA na kwa kura zao wataweza kuitoa CCM madarakani.
Mwenyekiti wa Baraza la Vinaja CHADEMA Taifa Mh Patrobas Paschal Katambi akihutubia mkutanoni hapo ambapo aliataka vijana kutokubali kuyumbishwa na wanasiasa wanaojaribu kuupotosha umma kuhusu ushirikiano wa vyama vinavyounda umoja wa UKAWA. Katambi alisisitiza zaidi kwa kutolea mfano wa ziara waliyonayo kwa pamoja na Mbunge Kafulila kuzunguka mikoa ya Kaskazini. Pia aliwataka vijana kuwatayari wakati wowote kupinga jaribio lolote la Serikali kuongeza muda wa kufanyika Uchaguzi Mkuu tofauti na mwaka huu.
Mh Godbless Lema akizungumza na wananchi wake hii leo ambapo alitumia muda mwingi kuwatoa hofu dhidi ya propaganda zilizoeneo Jijini hapa kwamba hatagombea Arusha Mjini tena na kwamba Jimbo la Arusha Mjini litarudi CCM. Lema aliwaambia wazipuuze propaganda hizo na kuziita ni za kipuuzi kwasababu hakuna namna ambayo CCM inaweza tena kuwashawishi wananchi wa Arusha kuichagua. Alisisitiza kuwa kwa muda mfupi aliowatumikia mbali na vikwazo vingi ameweza kutimiza wajibu wake kama mbunge kwa kiwango kikubwa huku akiorodhesha mambo mablimbali aliyotimiza kwa yeye binafsi na mengine kupitia madiwani wake.
Kwa pamoja, Mh David Kafulila na Mh Tundu Lissu walimuombea Mbunge Lema ruhusa kwa wananchi wa Arusha ili mbunge wao aendelee kufanya kazi ya siasa maeneo mengine nchini kuharakisha kile alichokiita ukombozi wa mara ya pili, na kwamba wasijikisike vibaya ama kudhani mbunge hakai nao Jimboni.
Waheshimiwa Kafulila na Lissu wakipokelewa na Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Arusha, Kalist Lazaro mwenye tisheti)
Viongozi wa CHADEMa na UKAWA wakiimba wimbo wa Taifa sambamba na wananchi (hawaonekani pichani) kabla ya kuanza hotuba zao
Kutoka kushoto waliokaa Mh Godbless Lema, Mh Tundu Lissu, Mh David Kafulila, Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Arusha Mh Kalist Lazaro na Mwenyekiti CHADEMA Wilaya ya Arusha Mjini Derick Magoma
Mh Kafulila akiteta jambo na Mh Lissu huku Mh Lema naye akiteta jambo na Mwenyekiti wa Vijana Arusha Mjini Mh Innocent Kisanyage
Mama na mwanae akiendelea kufuailia mkutano huku akisaidiwa kukingwa mvua
Mwenyekiti wa Vijana CHADEMA, Patrobas Katambi akisalimia wakazi wa Arusha waliojitokeza mkutanoni hapo baada ya kutambulishwa na Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema
Mh Kafulila akitamulishwa Jukwaani
Wananchi wakiuatilia mkutano huku mvua ikiendelea kunyesha
Mh Kafulila akisalimiana na Katibu wa CHADEMA Arusha Mjini Mh Lewis Kopwe. Wanaonekana walivyolowa chapa chapa
Wananchi wamelowa lakini hawaondoki mkutanoni
Mh Lissu akiwa amelowa mwili mzima na bado anaendelea kuhutubia huku mvua inayesha
Kutoka kushoto; Kalisti Lazaro, Patrobas Katambi, David Kafulila, Godbess Lema, Derck Magoma
Mwenyekiti na Katibu wa CHADEMA Arusha Mjini wakifurahia jambo
Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa (CHADEMA) ambaye pia ni mtangaza nia ya Ubunge Jimbo la Same Magharibi, Kamanda Chritopher Mbajo akiteta na Mwenyekiti wa Vijana CHADEMA Taifa Bw Patrobas Patambi, mwenye kombati
Mtia nia wa Jimbo la Mkalama Singida, Kamanda George Gunda (mwenye kombati nyeusi) kwa pamoja na viongozi wengine wakifuatilia hotuba ya Mh Tundu Lissu (haonekani pichani)
Mh Lema akiwatambulishwa viongozi wa Kata ya Ngarenaro na kueleza namna walivyoingilia kati hujuma ya kuchimbua uwanja huo mkutano usifanyike. Yupo diwani Doita
Msafara wa viongozi ukuindoka uwanjani hapo mara baada ya mkutano kumalizika. Wananchi waliwazonga kiasi cha kusababisha kazi ya ziada kwa wanausalama.
Eneo la uwanja wa Ngarenaro ambalo linadaiwa kupitishwa greda na wanaodhaniwa kuwa watu wa pinzani wa CHADEMA Jijini hapa kwa nia ya kujaribu kuzuia mkutano huu wa leo usifanyike eneo hilo, jaribio ambalo halikufua dafu kwani watu waliyapanda matuta hayo kama vile hakuna kitu na mwishowe kusawazika kiasi.
Bossi Mzito wa Blog Hii Akiteta Jambo naMwenyekiti wa BAVICHA Patrobas Katambi
PICHA ZOTE NA SERIAJr NA MAKABAYO
0 maoni:
Post a Comment