Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Taswira: Mkutano wa Lema na Kafulila Siha Kilimanjaro leo

WanaUKAWA machachari, Godbless Lema ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA na Mbunge wa Arusha Mjini pqmoja na Mbunge wa Kigoma Kusini kupitia NCCR, Mh David Kafulila hii leo wameanza ziara yao kwa Mikoa ya Kaskazini kwa kufanya Mkutano wa kwanza Wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro.

Wawili hao watakuwa na mkutano mwingine Mkubwa Jijini Arusha kesho Ijumaa katika viwanja vya Shule ya Msingi Ngarenaro kabla ya kuelekea mikoa mingine.

Moja ya mambo waliyosisitiza katika mkutano wa leo ni kuhimiza wananchi kujiyokeza kwa wingi kuandikishwa katika dafatari la kudumu la wapiga kura.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO