Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Diwani Bananga Akabidhiwa Kisima Cha Maji Kwa Shule ya Msingi Sombetini, Ufadhili wa Majaji wa Mahakama ya Kimataifa MICT

Diwani wa Kata ya Sombetini Jijini Arusha Mh Ally Bananga (mwenye tisheti nyeupe) hii leo amekabidhiwa rasmi kisima cha maji katika shule ya Msingi Sombetini kilichojengwa kwa ufadhili wa Waheshimiwa Majaji wa Mahakama ya Kimataifa (MICT), tukio ambalo ni matunda ya juhudi za Diwani huyo wa CHADEMA kuwatumikia wananchi wake.

Aidha, Mh Diwani alipokea pia msaada wa vyakula kwa ajili ya watoto yatima toka kwa rafiki wa maendeleo Neema Kaaya (dada wa Mh diwani Glory Kaaya).
Diwani Bananga akiwa katika picha ya pamoja na wafadhili hao pamoja na baadhi ya madiwani wenzake na viongozi katika eneo kilipo kisima hicho.
Picha pamoja baada ya kupokea msaada mwingine wa vyakula kutoka kwa mdau wa maendeleo Bi Neema Kaaya (mwenye blauzi nyeusi), vyakula mabavyo vitapelekwa kwa watoto yatima.
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO