Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

SERIKALI KUCHUNGUZA MKATABA WA JENGO LA MACHINGA COMPLEX

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaa, Paul Makonda akizungumza na wafanyabiashara katika Jengo la Machinga Complex Dar es Salaam jana, kuhusu uendeshaji wa jengo hilo.
 Makonda akiwasili katika viwanja vya Jengo la Machinga Complex kuzungumza na wafanyabiashara na wadau wengine. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi wengine ni viongozi wa jengo hilo.


Makonda akiangalia Uwanja wa Karume akiwa jengo la Machinga Complex.


Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, CP Simon Sirro akimuaga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda baada ya kumaliza kuzungumza na wananchi.

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaa, Paul Makonda (kulia), akikagua vizimba katika Jengo la Machinga Complex Dar es Salaam jana, baada ya kufanyika kikao cha kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa kilichoketi jana kujadili uendeshaji wa biashara wa katika jengo hilo pamoja na kamati ya mkoa iliyoundwa kuchunguza mkataba wa jengo.


Na Dotto Mwaibale

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameagiza kufanyika kwa uchunguzi katika ujenzi wa jengo la Machinga Ciomplex ili kubaini uhalali wa mkataba uliotumika kujenga jengo hilo.

Aidha, amebainisha kuwa jengo la Machinga Complex kwa sasa linadaiwa zaidi ya Sh bilioni 36 kiasi ambacho ni mara tatu ya thamani halisi ya jengo hilo ambayo ni Sh 12 ambazo zinatakiwa kulipwa na wafanyabiashara wa jengo hilo.

Makonda aliyasema hayo Dar es Salaam  jana wakati alipotembelea jengo hilo lililopo Manispaa ya Ilala ili kujionea mazingira ya kufanyia biashara. Alisema kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa itaanza kufanya uchambuzi wa mikataba ili kupata uhalali wa gharama na kujua kiwango kinachostahili kulipwa na wafanyabiashara hao.

Alisema kamati hiyo ya ulinzi na usalama imekubali kutengeza kamati ndogo itakayoanza kazi leo ya kuchambua na kuanza mikataba.

“Ingekuwa vyema tungekuwa na mkutano wa kuwasikilizeni na kujua kero zenu, lakini tunayo sababu moja ya msingi ya kutowasikiliza , kwanza tunatafuta uhalali na utaratibu wa jengo hili lilivyojengwa.

Katika maelezo ya awali tuliyoyapata jengo hili uko mkanganyiko mkubwa,  inawezekana ni miongoni mwa mradi mkubwa uliofanyiwa ufisadi Tanzania, sasa hatuwezi kukaa kusikiliza habari ya kizimba change, kwanza tupate uhalali wa mkataba uliopelekea kujenga jengo hili,” alisema Makonda.

Alisema kamati ya wafanyabiashara wa soko hilo itakayoundwa chini ya usimamizi wake itaanza kazi ya kuchunguza ili kubaini uhalali wa mkataba na kujua kama waliongia mikataba hiyo walikuwa sahihi.

Makonda alitoa rai kwa wafanyabiashara kuwa rai ya Rais Magufuli ni kuwapigania wanyonge na kuhakikish awanatoka sehemu moja kwenda nyingine, hivyo wasaidiza wake kwa kupenda au kutokupenda wana jukumu la kuhakikisha wanafanikisha hilo.

Hivi karibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, George Simbachawene aliifuta bodi inayosimamia jengo hilo na kumsimamisha kazi meneja anayesimamia jengo hilo na kumtaka kwenda katika ofisi za jiji kwa ajili ya kumpangia kazi nyingine.

Katika hatua nyingine, Simbachawene alilikabidhi jengo hilo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya kuandaa mpango wa kuwaingiza wafanyabiashara bila masharti huku ukiangaliwa utaratibu mpya kwa wafanyabiashara hao.



Katika mkutano wake na Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini, Simbachawene alisema, jengo hilo limekuwa likitumiwa kinyume na lengo ambalo walitakiwa wafanyabiashara kulitumia kwa gharama kidogo lakini limekuwa likitumiwa na watu wengine tofauti na wafanyabiashara jambo ambalo limesababisha kushindwa kulipa deni linalodaiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO