Diwani wa Kata ya Osunyai ya Jijini Arusha, Mh Elirehema Nnko (pichani kulia) akizugumza na wazazi na wananchi katika kikao cha mkakati kufanikisha sera ya Elimu Bure inafanikiwa kwa matokeo chanya ingawa sera hiyo inakabiliwa na changamoto kadhaa katika utekelezaji wake.
Kikao hicho cha wazi kilifanyikia Shule ya Sekondari ya Sombetini ambapo kwa pamoja na wazazi hao walikubaliana kuunda kamati ya Wazazi yenye wajumbe 10 ambayo itafuatilia na kubuni mikakati itakayohakikisha ufaulu wa wanafunzi unakuwa wa kuridhisha na itakapolazimu watoto wale shuleni.

Akifananua zaidi, Nnko amesema lengo la kamati hiyo ya wazazi waliyoichagua ni kuhakikisha elimu bure haiwi bure kweli kwa maana ya watoto kumaliza shule bila kuwa na ufaulu na maarifa yanayotakiwa.
Aidha, Diwani huyo aliwahimiza viongozi wenzake kushirikiana kwa mbinu na mikakati katika kutatua kero na changamoto zinazowakabili wananchi waliowaamini na kuwachagua kuwa viongozi wao.
Sehemu ya wananchi waliojitokeza katika mkutano huo wa wazi kujadili mustakabali wa elimu ya watoto wao
Pichani ni Diwani wa Kata ya Olasiti ya Jijini Arusha pia, Mh Alex Marti katika kutano mwingine wa wazi kuhusu mjadala wa Elimu Bure na changamoto zake na namna ya kuzitatua katika Kata ya Olasiti.
Baraza la Halmashauri ya Jiji la Arusha linaundwa na madiwani 24 wa kuchaguliwa kutoka Chama cha Demokrasia (CHADEMA) na Maendeleo na mmoja kutoka CCM ambaye ni Diwani wa Kata ya Kati, Mh Tojo. Pia wabunge wawili (mmoja wa kuchaguliwa Jimboni) na madiwani 8 wa viti maalumu kutoka CHADEMA

0 maoni:
Post a Comment