Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

WABUNGE WATAKA TANESCO ITUMBULIWE MAJIPU

Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Wabunge wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambao ni Wajumbe wa Kamati ya Viwanda na Biashara wamemtaka Rais John Pombe Magufuli kulitumbua jipu shirika la umeme Tanesco kwa kununua transfoma kutoka nje ya nchi licha ya kumiliki asilimia 20% ya hisa katika kiwanda cha Tansfoma cha Tanalec kilichopo jijini Arusha .
********

Kamati hiyo ya Bunge imebaini hayo jana  wakati wa ziara yao ya kutembelea viwanda jijini Arusha ili kufahamu changamoto na kasi ya ukuaji wa viwanda ambapo Wabunge hao wameshangazwa na kitendo cha Tanesco kutonunua transfoma katika kiwanda hicho ambazo huuzwa katika nchi jirani za Kenya ,Zambia Malawi na Burundi.

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara ,watatu kushoto Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dalali Kafumu,Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema na Vicky Kamata wakisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja uzalishaji wa kiwanda cha Tanalec Michael Laizer jana walipotembelea kiwanda hicho kilichopo jijini Arusha.Picha na Ferdinand Shayo

Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema ambaye ni Mjumbe wa Kamati hiyo alisema kuwa ni jambo la kushangaza kwa Tanesco ambao ni wamiliki wa Tanalec na wako katika wakurugenzi wa bodi lakini bado wanaagiza transfoma nje ya nchi suala ambalo linapaswa kutazamwa kwa umakini na kupatiwa majibu.

“Tunashindwa kuilewa Tanesco kwanini wanafanya hivyo wakati kiwanda ni cha kwao  na wakati Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco  Felchesmi Mramba  yuko ndani ya bodi ya wakurugenzi ,hapa kuna mgogoro ambao unapaswa kuatatuliwa kwa wakati ili kunusuru kiwanda hiki” Alisema Lema

Naye Mbunge wa Singida Mjini Musa Sima wamesema kuwa uamuzi huo wa Tanesco kununua  transfoma za nje ya nchi unazorotesha ukuaji wa viwanda vya ndani na kukiuka adhma ya Rais Magufuli ya kujenga uchumi wa viwanda nchini kwani ni vigumu kukuza viwanda wakati bila kuvilinda viwanda vya ndani dhidi ya bidhaa za nje.


Makamu Mwenyekiti wa  Kamati hiyo Vicky  Kamata  na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dalali Kafumu wameitaka serikali kuchukua maamuzi juu ya suala hilo la Tanesco ili kulinda viwanda vya ndani viweze kuchochea maendeleo ya Taifa.


Meneja Mkuu  wa Tanaleck Zahir Salehe ameiomba serikali irekebishe sheria za manunuzi ili zitoe kipaumbele kwa viwanda vya ndani viweze kukua na kutoa ajira nyingi hivyo kukuza pato la nchi.
Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO