Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TASWIRA: HALIMA MDEE AKIWA KATIKA MKUTANO WA KISIASA JIMBO LA MTAMA

Mwenyekiti wa Baraza la wanawake wa Chadema (Bawacha) na Mbunge wa Kawe Halima Mdee amemtaka Rais Dr. John Magufuli kuhakikishan anaweka wazi posho na marurupu anayoyapata ili watanzania wajue kiasi halisi anachokipata.
Mdee aliyasema hayo jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Sokoni Jimbo la Mtama Mkoani Lindi na kuhudhuriwa na wananchi wa Jimbo hilo.

"Juz Rais anasema eti mshahara wake 9.5 Millioni sasa atutajia Posho za kila siku ili kila Mtanzania ajue kiasi ambacho Rais anakipata na sio kudanganya wananchi,"alisema Mdee.
Mdee aliongeza kuwa wabunge wanalipwa mshahara Million3 lkn kuna posho mbali mbali kutokana na kuhudumia wananchi.
" Sisi wabunge mshahara wetu katika salary sleep unasoma Sh 3 Millioni lakini Posho na pesa ya mambo ya utendaji ya mbunge inafika 10 Millioni sasa Rais atuambie na yeye poshozake ni kiasi gani,"alisema Mdee.

Naye Mbunge wa Jimbo la Ndanda lililopoa Wilaya ya Masas Mkoani Mtwara Cecil Mwambe alisema kuwa wananchi wa Jimbo la Mtama wamekosa muwakilishi wa kuwasemea matatizo yao hasa ya upande wa kilimo cha korosho kutokana na Mbunge aliyepo Nape Nnauye hawez kusimama Bungeni na kuisema Serikali.

"Mtama mmekosa mwakilishi hapa kuna tatizo la korosho na mbunge aliyepo anashindwa kulisemea hivyo mtabaki hivyo hivyo bila kutatua tatizo lenu kwa kipindi cha Miaka Mitano,"alisema Mwambe
Hata hivyo mwenyekiti wa Bawacha anafanya ziara katika majimbo ya Lindi na Mtwara kwa kufungua matawi ya Chadema pomoja na kuongea na wanawake wa chama hicho.
Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO