Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

STARTIMES YAMLETA NCHINI MCHEZAJI KANU WA NIGERIA LEO MCHANA KUZINDUA DUKA JENGO LA MKUKI MALL ATAKUWEPO NCHINI KWA SIKU TANO


 Mchezaji wa zamani wa Nigeria, Nwankwo Kanu akizungumza na wanahabari baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam jana usiku kwa mwaliko wa siku tano wa Kampuni ya Vizimbuzi ya StarTimes.
 Mchezaji wa zamani wa Nigeria, Nwankwo Kanu alipokuwa akiwasili Uwanja wa Ndege.
 Hapa Kanu akihojiwa na wanahabari. Kushoto na kulia ni Mabaunsa waliokuwa wakimlinda baada ya kufika Uwanja wa Ndege kabla ya kuelekea Hoteli ya Serena.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania Be. Lanfang Liao (kulia), akimuelekeza jambo mchezaji huyo wakati wakielekea kupanda gari kuelekea Hoteli ya Serena. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Uhusiano wa StarTimes Tanzania,  William Masy.

Na Dotto Mwaibale

MCHEZAJI wa zamani wa Nigeria, Nwankwo Kanu jana usiku aliwasili nchini kwa mwaliko wa Kampuni ya Vizimbuzi ya StarTimes ambapo leo mchana anatarajia kuzindua duka la kampuni hiyo lililopo jengo la Mkuki Mall Barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam.

Kanu ambaye yupo nchini kwa ziara ya siku tano anatajaria kufanya shughuli mbalimbali za kijamii na kuzungumza na vyombo vya habari vya hapa nchini kabla ya kuondoka wiki ijayo kurudi kwao.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO