Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

HATIMAYE AMBULANCE YA MSAADA YA MBUNGE LEMA INAYODAIWA KUKATALIWA NA UONGOZI ULIOPITA KWA SABABU ZA KISIASA YAPOKELEWA NA MEYA WA JIJI KUTOKA CHADEMA


Gari hii iliyotengenezwa maalumu kwa kazi ya kubeba wagonjwa "Ambulance" imepokelewa rasmi hii leo na Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Mh Kalisti Lazaro kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Mh Godbless Lema. 


Awali ambulance hiyo iliwahi kukabidhiwa kwa uongozi uliopita ambao ulikuwa chini ya CCM lakini haikupokelewa kwa sababu zinazohisiwa kuwa za kisiasa.

Aidha, baada ya Mh Meya kukabidhiwa gari hiyo, aliikabidhi kwa Kata ya Moivaro ili iweze kusaidia wagonjwa wenye uhitaji kwa maeneo ya Kata za Moshono, Baraa, Kimandolu na Moivo. 

Pichani juu anaonekana Mstahiki Meya akiwa pembeni ya gari hilo mbele ya ofisi za Halmashauri ya Jiji la Arusha. 


Mh Meya Kalisti pamoja na madiwani wa Halmashauri, akiwemo Naibu Meya wa Jiji Mh Viola Likindikoki (mwenye gauni la zambarau)

Muonkano wa ndani wa Ambulance hiyo
Mh Meya akifurahia jambo na madiwani wake! 

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO