Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA INAYOONGOZWA NA CHADEMA YAFANIKISHA USAJILI WA KLABU YA JIJI "ARUSHA CITY SPORTS CLUB"

Hatua moja kuelekea kuwa na klabu ya michezo inayomilikiwa na Jiji la Arusha imefanikiwa ambapo Namba ya Usajili wa kalbu hiyo imekwishatolewa baada ya taratibu za kusajili kukamilika. Kabla ya Jiji la Arusha imepewa usajili nambari 11404 kuanzia tarehe 13/04/2015 kwa mujibu wa barua mabayo blogu hii imefanikiwa kuiona kutoka ofisi ya msajili wa vyama vya michezo Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo ambapo jina kalbu hiyo ni ARUSHA CITY SPORTS CLUB.

Mkakati wa Meya mpya wa Halmashauri hiyo kutoka CHADEMA Mh Kalisti Lazaro na Baraza lake la Madiwani ni kuwa na kalbu ya michezo ambapo pamoja na mambo mengine inalenga kuwa na kalbu binafsi ya mpira wa miguu itakayoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania maarufu kama Vodacom Premier League, ama kwa kukuza timu yao au kununua timu iliyokatika madaraja ya juu. 

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO