Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MKUU WA WILAYA YA ARUSHA AKUTANA NA MAKUNDI MAALUKU,ATOA MISAADA


Mkuu wa wilaya ya Arusha,Fadhili Nkurlu akimkabidhi mmoja wa watu wenye ulemavu wa ngozi,Kadi ya Bima ya Afya,Mafuta maalumu ya kutunza Ngozi na Kofia ya kujikinga na mionzi mikali ya jua,kulia ni Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu Tanzania(Chawata)mkoa wa Arusha,Said Kazigire.

Mkuu wa wilaya ya Arusha,Fadhili Nkurlu akimkabidhi mmoja wa watu wenye ulemavu wa ngozi,Kadi ya Bima ya Afya,Mafuta maalumu ya kutunza Ngozi na Kofia ya kujikinga na mionzi mikali ya jua,kulia ni Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu Tanzania(Chawata)mkoa wa Arusha,Said Kazigire.

Mkuu wa wilaya ya Arusha,Fadhili Nkurlu akimkabidhi mmoja wa watu wenye ulemavu wa kutokuona(Kipofu),Kadi ya Bima ya Afya itakayomwezesha kupata matibabu na wategemezi wake watano,kulia ni Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu Tanzania(Chawata)Said Kazigire.

Watu wenye ulemavu wa ngozi wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa wilaya ya Arusha,Ndg Fadhili Nkurlu

Mwenyekiti wa Chama cha wenye ulemavu wa Ngozi mkoa wa Arusha,John Kivuyo akizungumza katika mkutano huo.

Watu wenye ulemavu wa ngozi wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa wilaya ya Arusha,Ndg Fadhili Nkurlu.


Arusha.Mkuu wa wilaya ya Arusha,Fadhili Nkurlu ameitaka halmashauri ya Jiji hilo kutenga maeneo maulumu ya kuwawezesha wafanyabiashara wenye ulemavu kufanya shughuli za kujiingizia kipato badala ya kuwatumia mgambo wa jiji kuwabughudhi.

Nkurlu ametoa kauli hiyo kwenye mkutano na watu wenye ulemavu uliofanyika kwa lengo la kutambua changamoto zinazowakabili na namna ya kuzipatia ufumbuzi na kuwakabidhi kadi ya Bima ya Afya zitakazowawezesha kupata huduma za afya bure na wategemezi wao watano kwa mwaka .

Pia watu wenye ulemavu wa ngozi walipewa simu za mikononi 25 zilizotolewa na kampuni ya Halotel za kuwawezesha kuwasiliana pindi wanapohisi maisha yao yako hatarini,mafuta maalumu ya kulinda ngozi ,Kofia na Filimbi.

Alisema miundombinu katika nchi zinazoendelea imekua sio rafiki kwa watu wenye ulemavu na kukwamisha jitihada zao za kujikomboa na kuwa serikali itahakikisha watu wenye ulemavu wanapata haki zao kama wananchi wengine.

"Najua zipo asasi zilizoandikishwa kuwasaidia watu wenye ulemavu,lakini sio zote zinatimiza wajibu huo badala yake zinatumia nafasi hiyo kujinufaisha tutazichunguza na kuzifuta kabisa zisiwepo kwenye wilaya hii,"alisema Nkurlu

Ameitaka halmashauri ya jiji kutumia fedha zinazotengwa kwa makundi maalumu hasa wenye ulemavu ziwafikie walengwa badala ya kutumika kwa malengo mengine na kuagiza jiji linapofanya operesheni za kuwaondoa wanaofanya biashara kwenye maeneo yasiyo rasmi kuwatofautisha na wenye ulemavu.

Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu(Chawata)mkoa wa Arusha(Chawata)Said Kazigire alisema wanakusudia kufanya sensa ya watu wenye ulemavu ili kuwa na takwimu sahihi zitakazowasaidia kuwahudumia vyema.
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO