Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TANAPA KUZINDUA KAMPENI YA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO

Meneja Mawasiliano wa Tanapa ,Pascal Shelutete akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya kampeni ya kufanya usafi katika Hifadhi ya Mlima Kilimajaro akizungumza na Waandishi wa Habari jana katika Makao Makuu ya Tanapa,kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama cha Mawakala wa Utalii Sirili Akko,kushoto ni Afisa Masoko wa Hoteli ya Kibo Palace Jenipher.Picha na Stori: Ferdinand Shayo


Shirika la Hifadhi za Taifa TANAPA limejipanga kuzindua kampeni ya kitaifa ya  kufanya usafi mlima Kilimanjaro ambao unakusanya mapato ya shilingi bilioni 60 kwa mwaka na kuajiri Watanzania laki 3.

Meneja Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete akizungumza na Waandishi wa Habari amesema kuwa kampeni hiyo itasaidia kuboresha mazingira safi ya Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro na kuinusuru na uchafuzi wa mazingira wa kidunia (Global warming), Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), inatarajia kuzindua kampeni ya usafi wa mlima Kilimanjaro kesho ambayo itadumu kwa siku kumi.

“Tumeamua kufanya usafi katika mlima huo ikiwa ni jitihada za kuunga mkono juhudi za Rais John Pombe Magufuli katika kuweka mazingira katika hali ya usafi hususan hifadhi za taifa” Alisema Shelutete

Katibu Mkuu wa Chama cha Mawakala wa Utalii Sirili Akko amesema kuwa mashirika binafsi yaliyoko kwenye sekta ya utalii hayana budi kushiriki katika kufanya usafi katika mlima huo wa kwanza kwa urefu barani Afrika na wapili duniani.

Pia ameitaka serikali kusimamia maagizo ya Ofisi Makamu wa Raisi Mazingira kwa kupiga marufuku ya matumizi plastiki katika hifadhi za taifa ili kuepuka kuchafua mazingira.

Mdau wa Masuala ya Utalii ambaye ni Afisa Masoko wa Hoteli ya Kibo Palace Jenipher Swai amesema kuwa wameungana na Tanapa kufanya usafi kwa kutoa vifaa vya kufanyia usafi pamoja na kushiriki kupanda mlima huo katika madhimisho ya miaka kumi ya kuanzishwa kwa hoteli hiyo.

Jumla ya Watalii 50000 hutembelea Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro na kuchangia shilingi bilioni 60,kampeni ya kufanya usafi ya muda wa siku 10 itanza kesho ikiwashirikisha wapagazi,waongoza watalii na wadau wa utalii ,kuhakikisha hali ya usafi katika hifadhi zetu zitasaidia kuvutia watalii zaidi.

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO