Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

KATIBU WA CHADEMA MKOA WA DAR ES SALAAM AZUNGUMZA MIKAKATI MBALIMBALI YA CHAMA CHAO, AKEMEA UBAGUZI WA SERIKALI KWA WAPINZANI

 Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Dar  es salaam, Henry Kileo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo  juu ya mikakati mbalimbali ya chama hicho kulia ni Makamu  Mwenyekiti wa  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Dar es salaam, Benard Mwakyembe.
Makamu  Mwenyekiti wa  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Dar es salaam, Benard Mwakyembe  akizungumza na waandishi wa habari juu wananchi wanavyokosa habari wakati bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  kuto kuonyesha matangazo ya chama chao

(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii)

Chadema yalia na majipu na ubaguzi

CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimemtaka Rais John Magufuli kutumbua majipu makubwa yaliyokuwepo ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kufuata taratibu za uongozi kwenye utumbuaji huo,anaandika Faki Sosi.

Benard Mwakyembe, Kaimu Mwenyekiti wa Dar es Salaam kubwa(Great Dar es Salaam)ya Chadema amesema kuwa utumbuaji wa majipu mbele ya umma ni kinyume na taratibu za uongozi akitaja mfano wa kusimamishwa kazi hazalani kwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Wilson Kabwe sio utaratibu nzuri kwani angiitwa na kuchuunguzwa

“Ingawa ni vema kuwawajibisha viongozi wazembe lakini Rais anafanya maamuzi kwa mzuka wa ushabiki wa watu pasi nakufuta taratibu za uongozi”amesema Mwakyembe.

Mwakyembe amesema kuwa nyuma ya pazia la utumbuaji majipu kuna majipu makubwa ambapo utaratibu wa kuhojiwa kwa waliotumbuliwa utafanya kupatikana kwa mizizi ya majipu hayo.

“Nyuma ya Wilson Kabwe kuna Mstahiki Meya aliyemaliza Muda wake ambaye ni Didas Masaburi naye alipaswa kuwajibishwa kama mtuhumiwa kutokana na kuwa yeye ni mtu wa pili kusaini mikataba yote ya Jiji .

Na madiwani wote aliohusika na viongizi wote wa serikali wawajibishwe” amesema Mwakyembe.

Aidha alisema kuwa wamesikitishwa na kitendo cha Magufuli kutumia kumbagua Meya wa Jiji la katika ufunguzi wa daraja la Julius Nyerere maarufu kama daraja la Kigamboni baada ya kumfanya awe kama mvamizi kwenye uzinduzi huo.

Henri Kileo Katibu Mkuu Dar es Salaam Kubwa amesma kuwa Mkuu wa Mkoa ni kinara wa vitendo vya ubaguzi wa viongozi wa upinzani ili kuwadhoofisha .

Kadhia hiyo ya ubaguzi imehusishwa pia kwa Shirika la Taifa la Utangazaji (TBC) kutorusha matangazo au habari inayowahusu wapinzani.

Katibu Mkuu wa Great Dar es Salaam, alisema siku ya uzinduzi wa daraja hilo Mstahiki Meya alipokuwa anahutubia baada ya kupewa nafasi TBC walizima matangazo.

Mwakyembe anasema kuwa kwa shirika hilo kutorusha matangazo ya vyama vya upinzani sio mara ya kwanza kwani wao hawarushi matangazo ya aina yoyote yale yanayowalenga wapinzani

“ikiwa ile ni chombo cha habari cha taifa kinochoendeshwa kwa kodi za wananchi lakini wanahubiri ubaguzi ikiwa na vyama navyo ni vya walipa kodi vilivyosajiliwa kwa mujibu wa katiba.

Kama wanataka iwe hivyo basi waifanye TBC iwe kama Radio Uhuru ya CCM wananchi wajue kwamba ni shirika la utangazaji la CCM” amesema Mwakyembe.

MwanaHalisiOnline
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO