Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

JOSHUA NASSARI AJA NA MKAKATI WA KUONDOKANA NA MATUMIZI YA KUNI JIMBONI KWAKEMbunge wa Arumeru Mashariki Mh Joshua Nassai (CHADEMA) mwenye shati la bue nyeusi akiwa na baadhi ya viongozi na wataalamu wa BioGas katika kujifunza namna gesi itokanayo na kinyesi cha mifugo hususani ng'ombe na kuweza kutumika kupunguza matumizi ya kuni katika Jimbo la Arumeru.

Mbunge Nassari ameazimia kuipigania teknolojia hii kuweza kutumika jimboni kwake ili kuweza pia K
uokoa Mazingira, Kuboresha maisha ya wana Meru na wakati huo huo mbolea hiyo hiyo inayozalisha gesi asilia kutumika shambani.

Blogu hii inathamini sana ubunifu wa aina hii na tunampongeza mheshimiwa mbunge kwa kuifikiria zaidi jamii yake na taifa kwa ujumla.


Moja ya mtambo wa kuzalisha Bio Gas/ Bio-fuel Arumeru Mashariki.

Pich ya pamoja baada ya ukaguzi na mafunzo

Picha zote na Ofisi ya Mbunge, Arumeru Mashariki

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO