Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

WASANII KUIGIZA FILAMU WAHIMIZWA KUTUMIA MANDHARI ZA HIFADHI BADALA YA YA MJUMBA YA KIFAHARI KUREKODI KAZI ZAO ILI KUSAIDIA KUTANGAZA UTALII WA NCHI


Wasanii wa Filamu nchini kote wametakiwa kutumia mandhari za asili zilizoko katika maeneo ya  hifadhi za taifa kwenye shughuli zao za kurekodi filamu badala ya kutumia majengo ya kifahari ili kutangaza utalii kwa kupitia kazi zao.

Hayo yameelezwa na Meneja Mawasiliano wa  Shirika la Hifadhi za Taifa TANAPA ,Pascal Shelutete wakati akizungumza katika Tamasha la Chama Wasanii wa filamu  jijini Arusha (TDFA) lililofanyika  katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid .

Shelutete amesema kuwa Tanapa itatoa ushirikiano kwa wasanii watakaoonyesha nia ya kurekodi filamu zao katika maeneo ya hifadhi ambayo ni salama nay a kuvutia yenye maparomoko ya maji na mandhari za kuvutia ambazo zitasaidia kuhamasisha utalii ambao kwa sasa unaongoza kuchangia pato la taifa.


Mwenyekiti wa Chama cha Wasanii hao Fredrick Kefas amewataka wasanii kutumia taaluma yao katika kuhimiza utalii wa ndani utakaoliingizia taifa pato kubwa na kuinua uchumi wan chi hivyo kuondokana na utegemezi.

Rais wa Shirikisho la Filamu nchini (TAFF) Simon Mwakifamba amewataka Wasanii kutumia vizuri fursa ya maonyesho ya kimataifa ya filamu yanayojulikana kama  Tanzanite  International Film Festival yatakayojumuisha wasanii mahiri wa filamu kutoka nchi mbalimbali duniani ikiwemo Marekani,Asia ,Australia .


Alisema Tamasha la Wasanii wa  Filamu jijini Arusha lilipambwa na michezo mbali mbali ikiwemo timu ya mpira wa miguu ya wasanii wa Kilimanjaro na Wasanii wa Arusha,timu za mpira wa miguu za mkoani Arusha  pamoja na mchezo wa netiboli,Michuano bado inaendelea ambapo mshindi wa kwanza atapata fursa ya kutembelea Hifadhi ya Manyara na Ngorongoro.

Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO