Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

HABARI NA PICHA: UZINDUZI WA KITUO CHA POLISI CHA TENGERU


Vituo vingi vya polisi hasa vile vilivyopo pembezoni mwa miji vimekua vikikabiliwa na changamoto ya uchakavu wa majengo,uhaba wa majengo pamoja na vitendea kazi suala ambalo linapunguza kasi ya jeshi la polisi katika kupambana na uhalifu.


Hayo yameelezwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha aliyemaliza muda wake Liberatus Sabas amesema kuwa uhaba wa majengo na vituo katika maeneo ya vijiji umekua ukipunguza ufanisi wa kazi ya polisi katika kulinda raia na mali zao hivyo ameitaka serikali kukarabati vituo hivyo pamoja na kuweka vitendea kazi vya kutosha.

Akizungumza katika uzinduzi wa kituo kipya cha polisi cha Tengeru kilichozinduliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Daudi Felix Ntibenda amesema kuwa hatua ya kuboresha vituo vya polisi itasaidia kutatua kero za kiusalama zinazokabili maeneo mengi mkoani Arusha.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Meru amelitaka jeshi la polisi kuwachukulia hatua baadhi ya polisi ambao huwabambikia wananchi na kujihusisha na vitendo vya rushwa ambavyo huwaumiza wananchi wengi.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha aliyezindua kituo hicho amewataka Wananchi wa kushirikiana vyema na jeshi la polisi katika kutoa taarifa za uhalifu ili kutokomeza vitendo vya uhalifu vinavyojitokeza kila mara

Na  Ferdinand Shayo,Arusha.
Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO