Juma hili Blog hii iliweka bandiko la kijana Godlisten Malisa kuhusiana na sakata la Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh Zitto na hatma yake kisiasa ndani ya CHADEMA.
Tumepata taarifa kuwa bandiko hilo lililochapishwa na Malisa kwenye mtandao wake wa Facebook lilichukuliwa na Gazeti la Rai na kuchapishwa na gazeti hilo toleo la jana Alhamisi Machi 19, 2015kama makala bila ridhaa ya mhusika.
Ndugu Malisa amenukuliwa mahali na Blog hii akilalamika “Nimeshtushwa, sikua na mawasiliano yoyote na RAI kabla ya hapo. Nachoweza kusema ni kuwa RAI wamekiuka maadili ya taaluma ya habari na walichofanya si uungwana. Licha ya kwamba wameniackowledge kwenye makala hiyo lakini walipaswa kunijulisha kwanza. Kwa hiyo NAPINGA VIKALI kuhusika na uchapaji wa makala hiyo RAI, napinga kutoa ridhaa ya uchapaji na pia nalaani kitendo hicho kwani kinakwenda kinyume na maadili ya habari. Niko tayari kuchukua hatua za kisheria…. Huwezi kukuta andiko la mtu tu mahali halafu ukacopy na kupaste kwenye gazeti lako na kuiita habari. Thats is not fair at all. Nachoweza kusema RAI hawajanitendea haki.!”
Andishi husika ni hili hapa kwenye ukurasa wa Malisa Facebook na kama tulivyouripoti kwenye Arusha255 hapa
0 maoni:
Post a Comment