Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MAKUNDI YA KIJAMII YAZIDI KUMSHAWISHI LOWASA KUGOMBEA URAIS

 

Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akiwasalimia mamia ya wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu mkoa wa Dodoma, waendesha boda boda na wamachinga wa mkoa huo walioandamana hii leo hadi nyumbani kwake Area D mjini Dodoma kumuomba pindi wakati ukifika kwa mujibu wa taratibu za chama cha Mapinduzi (CCM) asisite kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Urais.

Lowassa amesema anazidi kuhamasika kufuatia maombi ya watu wa makundi mbalimbali ya jamii wanao muomba kugombea urais mwaka huu. Aidha na yeye amewaomba vijana hao na makundi mengine kuwahimiza wenzao vyuoni na hata mitaani kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la wapiga kura ili siku ya uchaguzi wawe na sifa za kuweza kushiriki katika uchaguzi kwa kupiga kura.

Wanafunzi hao zaidi ya 300 walifika nyumbani kwake hapo majira ya saa sita mchana na kuzungumza nae na kufikisha salamu zao ikiwa ni pamoja na kumchangia fedha za kuchukulia fomu.

Aidha Lowassa kwa Upande wake amewashukuru vijana hao na kusema kuwa ujio wao na ule wa masheikhe wa Bagamoyo unazidi kumhamasisha kutangaza nia na pindi muda ukifika anaweza kufanya hivyo.

Walibeba na mabango yaliyo na jumbe mbalimbali

Bodaboda nao walifika eneo hilo

Sehemu tu ya umati uliofika nyumbani hapo kwa Lowassa hii leo

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO