Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Joyce Mukya “awajaza mapesa” wamama wa Arusha

1600MBUNGE wa viti maalumu , Joyce Mukya kupitia taasisi yake ya JoyFoundational ameanzisha mpango wa kuwakwamua kiuchumi wanawake wa jiji

la Arusha kwa kuwapatia msaada wa fedha kupitia vikundi vyao vya

ujasiriamali watakazo zitumia kukopeshana.

Akizungumza na gazeti hili wakati akikabidhi fedha tasilimu kwa akina mama waliopo katika kata za Sakina,Sombetini na Engutoto jijini

Arusha,alisema msaada huo utawasaidia wakina mama kujiajiri wenyewe

kwa kufanya biashara ndogo ndogo na kwamba hata hitaji kureejeshewa

fedha hizo .

Alisema anajisikia uchungu kuona mwanamke akiteseka kutokana na majukumu mengi ikiwemo kulea na kusomesha watoto huku waume zao

wakiendekeza starehe za unywaji wa pombe bila kujali famila zao.

Alisema hali hiyo ndio imemsukuma na kuamua kutenga zaidi ya shilingi milioni 20 na kuzigawa kama msaada kwa wanawake watakao kuwa

wamejiunga kwenye vikundi katika kata zote 28 za jijini Arusha.

''Nimeamua kutoa mchango wangu kwa wanawake kama sehemu ya majukumu yangu kama mama nina mtoto ninaleaa najua shida za mwanamke ,hizi

fedha sio kwamba sizihitaji ila lengo langu ni kumkwamua mwanamke

mwenye uhitaji''alisema Nkya.

Aidha alisema tayari ameshatoa kiasi cha shilingi milioni 6.5 katika kata nne za jiji la Arusha ,ambapo kata ya Moshono aliwapatia kikundi

cha akina mama shilingi milioni 1.5 kati ya million 3 alizoahidi,kata

mpya ya Sakina sh, milioni 1.5,kata ya Sombetini sh,milioni 2 na kata

ya Engutoto sh,milioni 1.5.

Alisema lengo lake ni kuona fedha hizo zikistawi na kuwanufaisha wanawake wengi zaidi jijiji haapa na baadae kuongeza zaidi mfuko wao

ili kupanua wigo wa kukopeshana

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO