Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TASWIRA: HESHIMA ZA MWISHO KWA MAREHEMU KAPTENI JOHN KOMBA VIWANJA VYA KARIMJEE JIJINI DAR ES SALAAM

Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Kapteni John Komba likiwa limebebwa kuelekea kwenye jukwaa maalum kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Familia ya Marehemu Kapteni John Komba ikiwa imesimama tayari kuupokea mwili wa marehemu kwenye viwanja vya Karimjee.

Ni huzuni kubwa kwa familia ya marehemu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akiwa pamoja na Makamu wa Rais Ghalib Bilal (kushoto) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anna Makinda wakiwa kwenye viwanja vya Karimjee ambapo mwili wa Marehemu Kapteni John Komba uliagwa na Viongozi mbali mbali na wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akis

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akizungumza na   Makamu wa Rais Ghalib Bilal kwenye viwanja vya Karimjee ambapo mwili wa Kapteni John Komba ulikuwa unaagwa .

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye  akiimba wimbo maalum wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Kapteni John Komba aliyefariki tarehe 28 februari 2015 jijini Dar es Salaam.

Viongozi wa CCM pamoja na wanamuziki wa muziki wa dansi wakiimba kwa pamoja nyimbo maalum wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Kapteni John Komba.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoa heshima ya mwisho kwa marehemu Kapteni John Komba .

Mzee Yusuf Makamba akifutmachozi wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Kapteni John Komba

Kada wa CCM na Mwanasiasa mkongwe nchi Kingunge Ngombale Mwilu akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Kapteni John Komba

Katibu wa NEC Idara ya Oganaizesheni CCM Dk. Mohamed Seif Khatib akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Kapteni John Komba

Waziri wa Mambo ya Nje na uhusiano wa Kimataifa Bernad Membe akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Kapteni John Komba

Viongozi na wananchi kutoka sehemu mbali mbali wakiwa kwenye foleni ya kwenda kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Kapteni John Komba kwenye viwanja vya Karimjee.

Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Arusha Mheshimiwa Catheline Magige akiondoka eneo la tukio baada ya kumaliza kutoa heshima zake za mwisho kwa marehemu Kapteni John Komba Ungana na HAKI NGOWI KWA KUBOFYA HAPA

KWA PICHA NA MATUKIO MENGINE YA AWALI UNGANA NA MICHUZI MEDIA HAPA

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO