Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Ukatili Arusha - Mwanamke Akodiwa Watu Wakamuingizia Chupa ya Bia Sehemu za Siri

Taarifa ambazo zimeifikia Blog hii zinaeleza tukio baya la ukatili kwa mwanamke lililotokea wiki hii Jijini hapa.

Kuna ukatili wa kutisha ambapo Mwanamke mmoja anatuhumiwa kukodi wanawake wanne wakamwingizia chupa ya bia mwananmke mwenzao kwenye sehemu nyeti hadi kizazi kikatoa damu.

Taarifa zinadai kuwa mtuhumiwa aliyetekeleza tukio hilo alikamatwa na Polisi lakini kwasasa yupo nje kwa dhamana licha ya hali mbaya  ya mwathirika.

Uchunguzi wa Blog hii kuhusu sakata hilo umegundua kuwa mtuhumiwa na aliyeingiziwa chupa (majina yao yanahifadhiwa) ni majirani mmoja anaelezwa kuwa na Pub maeneo ya Arumeru Sokoni jirani na Apache Bar mwenzake ana Salon.

Inaelezwa kuwa huyo mwenye Pub alimwita wa Salon ndani kwake na alipoingia akakuta wasichana wanne, wakamshika na kumwingizia chupa ya bia sehemu za siri kisha wakamwachia na kumtishia kuwa asidhubutu kusema. Aliporudi kwake hali ikawa mbaya sana ndio akawajulisha ndugu zake kisha kumpeleka polisi halafu hospitali.

Mtuhumiwa alikamatwa na kuwekwa ndani siku moja tu siku iliyofuatia akaachiwa polisi wakadai kuwa sio vizuri mwanamke aliyekwenye hedhi akae lock up.

Mwathirika yupo hospitali ya Mount Meru na hali yake inaelezwa sio nzuri sana.

Jambo baya zaidi, inadaiwa mwanamke huyo alichukuliwa picha za video wakati anaingiziwa chupa.

Baadhi ya watu waliozungumza na Blog hii kuhusiana na kadhia hiyo wamesisitiza taasisi zinazoshughulikia mawala ya ukatili kwa wanawake waingilie kati. Miongoni mwao ni pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA) Mkoa wa Arusha, Mh Cecilia Ndossi ambaye ameahidi kulifuatilia swala hilo kwa ukaribu ili kuona sheria inafuatwa na haki kutendeka.

Washirikishe Google Plus

About Ujenzi Connekt

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO