Hivi karibuni Mbunge wa Arusha Mjini kupitia CHADEMA, Mh Godbless Lema alizungumza na waandishi wa habari kuzungumzia mrejesho wa ahadi zake mbalimbali kwa wananchi na kueleza kuwa ahadi yake kujenga hospitali ya kina mama na watoto bado iko pale pale na utekelezaje wake unadndelea. Lema alisema hivi karibuni ujenzi wa hospitali hiyo ya mama na mtoto utaanza ambao utajumuisha ujenzi wa chuo cha uuguzi kwani michoro ipo tayari na utagharimu dola milioni 3.2, huku kiwanja kikiwa tayari kwa mradi huo eneo la Burka.
Lema alisema ahadi ya kulipia ada watoto masikini, yatima na wale wanaoishi kwenye mazingira magumu aliitekeleza mwaka 2011 ambapo aliwalipia ada watoto 400 kwa usimamizi wa ArDF (Arusha Development Fund). Alisema mwaka uliofuata akiwa na kesi ya ubunge alifanya ushawishi kwenye Halmashauri ya Jiji la Arusha ili waendeleze utratibu huo na aliyekuwa Mkurugenzi aliridhia kuwaandikia barua wakuu wa shule za Sekondari waendelee na masomo na hakuna mzazi aliyemfuata kulalamika mpaka sasa.
Picha ya kwanza juu: Tukio la mwaka 2013 mwezi Februari ambapo Lema alikabidhiwa shamba na mwakilishi wa kampuni ya Mawalla Advocates kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa hospitali ya Mama na Mtoto eneo la Burka Jijini Arusha. Hapa anaonekana akipikea mkataba wa makabidhiano.
Picha ya pili ni Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mh Freeman Mbowe akizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano ya shamba hilo huku Mwenyekiti wa BAWACHA mKoa Bi Cecilia Ndossi akiduatilia pamoja na viongozi na wawakilishi wa Mawalla Advocates.
Picha na Seria Tumaini; Arusha
Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema (kushoto) akihutubia katika hafla ya kukabidhi msaada wa ada na kadi za afya kwa watoto 400 wenye uhitaji jimboni Arusha Mjini, hafla hiyo ilifanyika nje ya ofisi za Mbunge huyo, kulia kwake ni mwenyekiti wa mfuko wa maendeleo ya jimbo la Arusha Mjini(ArDF), Elfuraha Mtowe
Mbunge wa jimbo la Arusha mjini,Godbless Lema (mwenye tai nyekundu) akijumuika na watoto 400 wenye uhitaji ambapo walikabidhiwa ada pamoja na kadi za afya nje ya ofisi za mbunge huyo, jumla ya kiasi cha shilingi milioni 60 ziligharimu mahitaji hayo.
Picha za ArDF kutoka Maktaba na Joseph Ngilisho, GPL/ Arusha
0 maoni:
Post a Comment