Ndugu zangu, nimejulishwa na viongozi wetu wa Zanzibar juu ya kushambuliwa kwa wafuasi wa CUF waliokuwa kwenye harakati za chama huko makunduchi (Picha imeambatanishwa hapa). Hali hii ni dalili mbaya wakati tunaelekea mwezi Oktoba mwaka huu.
Ni jambo lisilofichika kuwa vyama vyote (CCM na CUF) vinapaswa kukaa chini na kuweka utaratibu ambao utaifanya Zanzibar iingie kwenye uchaguzi mkuu bila damu ya mtu hata mmoja kumwagika.
Haiwezekani katika karne hii bado watu wanaishi kwa kubaguana, kwa kulipiziana visasi na kuumizana. Huu ni wakati wa kujenga demokrasia Zanzibar na kuwaachia wazanzibari mamlaka ya kuchagua viongozi wawatakao.
Na huu ni mwaka ambao Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) inawajibika kumtangaza Rais halali atakayechaguliwa Zanzibar.
Huu ni mwaka ambao wapiga kura na wafuasi wa vyama vyote viwili hawapaswi kutishwa ili wasishiriki kufanya maamuzi mwezi Oktoba mwaka huu.
Kama tunaona amani ni ghali, basi tuchague vurugu!
0 maoni:
Post a Comment