Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MO DEWJI FOUNDATION YAMPATIA BAISKELI KIJANA ALIYEPOOZA MGUU

Na Andrew Chale wa Modewji blog

“Hujafa, hujaumbika naamini hilo, kwani awali nilikuwa najitafutia riziki zangu za kujikimu kimaisha lakini nilipopata tatizo hili la kupooza mguu na kulemaa ndoto zangu zote zimeyeyuka ila sijakata tama” Hivi ndivyo anavyomalizia Paulo Ezekiel ambaye anaishi Mbagala, Temeke Jijini Dar es Salaam, Tanzania.

DSC_0370

Mtendaji Mkuu wa MO DEWJI FOUNDATION, Gerald Mgesi David akimkabidhi rasmi kijana Paulo Ezekiel (23) msaada wa baiskeli ya magurudumu matatu (tricycle) itakayomsaidia katika kutembelea kwenye shughuli zake za kila siku.

 

Taasisi ya MO DEWJI FOUNDATION   inayojishughulisha na miradi ya kusaidia jamii Tanzania katika masuala mbalimbali ikiwemo Afya, elimu na maji mwishoni mwa wiki imeweza kumpatia  kijana Paulo Ezekiel (23) msaada wa baiskeli ya magurudumu matatu (tricycle) itakayomsaidia katika kutembelea kwenye shughuli zake za kila siku.

Tukio hilo la makabidhiano limefanyika katika ofisi za Mo Dewji Foundation jijini Dar es Salaam ambapo Mtendaji Mkuu wa MO DEWJI FOUNDATION,  Gerald Mgesi David alikabidhi msaada huo kwa kijana Paulo Ezekieli

DSC_0397

Mwandishi wa habari wa modewjiblog, Andrew Chale (kushoto) akifanya mahojiano na Paulo Ezekiel mara baada ya kukabidhi msaada wa baiskeli ya magudumu matatu.

Kijana huyu awali alikua akifanya shughuli za kutafsiri Lugha kwa wageni wanaokuja kununua bidhaa kwenye maduka ya Kariakoo na Bandari ya Dar es Salaam hasa wafanyabiashara wanaotoka Congo, Rwanda, Zambia, Malawi, Burundi na maeneo mbalimbali.

Paulo Ezekiel ni mtoto wa pili kati ya watoto nne, anatokea Mkoa wa Kilimanjaro na kabila lake ni Mchaga.

DSC_0317-1024x682

MO DEWJI FOUNDATION: Ni taasisi iliyoanzishwa na Mbunge wa Singida Mjini (CCM) na mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji  maarufu ‘MO’ (pichani) ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya kiongozi bora aliyejitolea kwa kiasi kikubwa katika jamii na kuleta mabadiliko Afrika kwa mwaka 2014.

Tuzo hiyo  aliyotunukiwa MO iitwayo African Philanthropist of the year Award 2014, Ilitolewa na jarida la uongozi la Uingereza, jijini Dubai wakati wa Jukwaa la Viongozi wa Afrika.

Kabla ya kukabidhiwa tuzo hiyo,  sifa kuu aliyokuwa nayo MO  kama alivyofafanua wakati wa kukabidhiwa tuzo hiyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa jarida hilo, Dk Ken Giami alisema wataalamu waelekezi walimchagua Dewji kuwa mshindi kutokana na:  Uongozi  bora katika Kampuni yake ya Mohammed Enterprises (MeTL GROUP) Pia  kigezo kingine kilichompa ushindi ni namna anavyojihusisha na kazi mbalimbali za kijamii.

Pia Mchango  wa MO  katika elimu ni sehemu kubwa ya mafanikio yake  hususan kwa kuendeleza ujenzi wa shule mbili hadi 12, pamoja na kujitolea  kiasi cha zaidi ya Sh520 milioni katika kuendeleza sekta hiyo ya elimu ndani ya jimbo lake hilo la Ubunge la Singida Mjini.

MO pia amekuwa akisaidia sekta ya afya kwa ushirikiano na Taasisi ya Bilal Muslim Mission ya Tanzania kwa kuwaleta madaktari waliowafanyia upasuaji wagonjwa  wa macho na 179 kupata miwani,  kusambaza maji safi na salama kwa kuchimba visima vingi vya maji ndani ya jimbo na n.k.

Kwa sasa MO ndie Bilionea kijana Afrika kwa mujibu wa jarida la Forbes. Unaweza kusoma zaidi kupitia http://www.forbes.com/profile/mohammed-dewji/

Kwa hali hiyo pia Dewji ameingia katika orodha ya Philanthropist duniani pia waweza kuona watu wengine waliotunukiwa tuzo kama hiyo kupitia hapa: http://en.wikipedia.org/wiki/List_of_philanthropists

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO