Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TASWIRA YA MKUTANO WA PAMOJA WA VYAMA VINAVYOUNDA UMOJA WA KATIBA YA WANANCHI UKAWA JIJINI WASHINGTON DC, MAREKANI

 

Viongozi wa Vyama vya CUF na CHADEMA wakiwa pamoja katika mkutano jijini Washington DC.

Mbunge wa Mji Mkongwe Zanzibar Mh Ismail Jussa akiwa katika mkutano wa Pamoja wa Vyama vinavyounda umoja wa Katiba UKAWA jijini Washington DC.

Viongozi wa CUF na CHADEMA DMV wakiwa na Mgeni rasmi Mh Ismail Jussa.

Kutoka Kushoto ni Mbunge wa Mji Mkongwe Zanzibar Mh Ismail Jussa, wa pili ni Mh Shamis ambaye ni Mwenyekiti wa CUF DMV, wa tatu ni Mwenyekiti wa CHADEMA DMV Kalley Pandukizi na wa nne ni Katibu wa Tawi la CHADEMA DMV Liberatus Mwang'ombe.


Katibu wa Tawi la CHADEMA DMV Liberatus Mwang'ombe akiongea katika Mkutano wa pamoja unaunganisha vyama vya CUF na CHADEMA.


Mwenyekiti wa CHADEMA DMV Kalley Pandukizi akiongea kabla ya Kumpisha Mgeni Rasmi Mh Ismail Jussa.


Mh Jussa akiwa na Mwenyekiti wa Tawi la CHADEMA DMV Kalley Pandukizi.

Viongozi wa CHADEMA na CUF DMV wakiwa na Mh Jussa katika Picha ya Pamoja kuonyesha Mshikamano wa Vyama vyao.

Kutoka kushoto ni Katibu Mwenezi wa Tawi la CHADEMA DMV Ndugu Hussein Kauzela, katikati ni Mh Ismail Jussa na Kulia ni Katibu wa CHADEMA DMV katika picha ya pamoja kuonyesha mshikamano.

Mwenyekiti wa CUF DMV Ndugu Shamis akiwa na Katibu wa Baraza la wanawake Ndugu Baybe Mgaza.

Katibu Mwenezi wa CHADEMA DMV Ndugu Hussein Kauzela akiwa na Mweka Hazina wa Tawi la CHADEMA DMV Ndugu Ludigo Mhagama.

Mh Ismail Jussa akiwa na Kada wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Salma Moshi.

Kwa Picha zaidi Bonyeza Kishale Hiki »

  ***************************************

JUSA: SUALA LA KABTIBA HALIJAFIKIWA KAMA WANANCHI WANAVYOTAKA

Na Abou Shatry Washington DC  Anaripoti

Mwakilishi wa jimbo la mji mkongwe wa chama cha wananchi CUF Mhe: Ismail Jussa Ladhu amesema Tanzania inaelekea kusipotarajiwa na maoni waliyotoa wananchi kwa ajili ya Bunge la Katiba.

Muwakilishi wa jimbo la mji mkongwe Mhe: Ismail Jussa Ladhu akiongea na waTanzania wa DMV Siku ya Jumamosi Feb 28, 2015 kwenye ukumbi wa Tabeer Hall uliopo University Blvd East, Hyattsville, Maryland, Nchini Marekani.
Aidha amesema matarajio ya watanzania hayajatimizwa mbali ya kuwepo mijadala mingi juu ya rasimu ya Jaji Warioba ili kulipatia ufumbuzi wa kudumu Suala  la katiba mpya.
Mhe. Jussa aliyasema hayo wakati akizungumza na Watanzania wa DMV siku ya Jumamosi Feb 28, 2015 kwenye ukumbi wa Tabeer Hall 1401 University Blvd East, Hyattsville, Maryland, Nchini Marekani.
Pia Mhe. Jussa ambaye pia ni mjumbe wa UKAWA amesema uamuzi wa UKAWA kususia na kujitoa katika bunge la katiba ni kwa sababu chama tawala CCM kimekwenda kutetea sera zake na kupinga mawazo ya wananchi ambayo yamewakilishwa katika rasimu ya Jaji Warioba.
Mkutano huo ulijumuisha Agenda kadhaaha ikiwemo Mchakato wa Katiba mpya, Ufafanuzi juu ya muundo wa serikali tatu, Uamuzi wa UKAWA kususia mchakato huo dhalimu na sababu ya maoni ya watu walio Diaspora kuhusu Uraia Pacha kutokutekelezwa kama walivyotarajia.

Watanzania waishio DMV(Washington DC, Maryland na Virginia) wakimsikiliza Mh Ismail Jussa alipohutubia katika mkutano uliondaliwa na Muungano wa Vyama vya CUF na CHADEMA Marekani.

Mwakilishi wa jimbo la mji mkongwe Mhe: Ismail Jussa Ladhu akiongea na waTanzania wa DMV, walioka meza kuu wakanza kushoto Katibu wa Tawi la Chadema DMV Liberatus "Libe" Mwangombe, akifuatiwa na Mwenyekiti wa Tawi la Chadema DMV Mhe. Kalley Pandukizi, Shamis Alkhatry CUF pamoja na Katibu Mkuu wa Baraza la kina mama CHADEMA DMV Bi Baybe Mgaza.

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO