Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

FM ACADEMIA 'WAZEE WA GWASUMA’ KUWASHA MOTO WILAYANI HAI USIKU WA JUMATATU YA PASAKA

 

Na Woinde Shizza,Arusha

Bendi ya FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma wanatarajiwa kuwasha moto  ndani ya ukumbi mpya wa kisasa  ujulikanao kwa jina la Flomena uliopo  wilayani hai mkoani Kilimanjaro usiku wa jumatatu ya pasaka .

Akizungumza na waandishi wa habari muandaaji wa onyesho hilo  Swaum Kileo alisema kuwa ameamua kuwaleta bendi hiyo katika uzinduzi huo ili kuweza kuwafurahisha wananchi wa mkoa wa kilimanjaro na mikoa jirani katika sikukuu hiii ya pasaka .

Alisema kuwa  bendi hii inamda mrefu sana aijafika wilayani hai ivyo wameamu kuileta ili wakazi wa wilaya hiyo nao wafurahie mziki wa dance unaofanywa na bendi hiyo .

Alitaja kiingilio cha onyesho hiyo kuwa ni shilingi 10000 za kitanzania huku akiwataja wathamini wa onyesho hilo kuwa ni Swaum fashion ,Tbl , libeneke la kaskazini blog pamoja , faraja saloon  pamoja na Radio five.

Kwa upande wa meneja wa bendi ya FM Academia kelvin  mkinga aliema kuwa wamejipanga vyema kuwapa burudani ya kutosha wakazi wa wilaya ya hai mkoa mzima wa Kilimanjaro pamoja na mikoa jirani  na kwa upendeleo watawatambulisha nyimbo zao mbalimbali mpya ambazo wameziandaa na wanatarajia kuzi zindua hivi karibuni.

Alisema kuwa pia wapenzi wake watakuwa na bahati zaidi kwani   show hii ndio itakuwa ya kwanza mara baada ya kutoka katika  shindano lao na bendi ya twanga pepeta kwa upande wa Rais wa bendi hiyo Nyoshi El-Sadat   alisema kuwa timu  yake yote imejipanga vyema kuwapa burudani ya nguvu wakazi wa wilaya ya hai na mkoa mzima huku akisema  kuwa atawapa staili zote za gwasuma ikiwemo ile ya   vundesa  ambapo alisema kuwa wameiboresha na imekuwa ya kiufasaha  zaidi  na ina vinjonjo vingi zaidi ,staili tamu  pamoja na maneno matamu.

“tunatarajia kufanya show  ya kihistoria ambayo aijawai kufanyika  mkoani Kilimanjaro nah iii yote ni kwa ajili ya kuwaburudisha wapenzi wetu wa mziki wa dance wapenzi wetu wa bendi yetu ya fm academia”alisema nyoshi

Aidha alisema kuwa amewaandalia zawadi kubwa wapenzi wake wa mkoa wa huo  pamoja na mikoa jirani kwani watamuoana akiwa na muonekano mpya ambao hawajawai kuuona.

ni pamoja na kuwaelewesha wapenzi wao nyimbo mpya na kuakikisha wapenzi wao wanajua staili zao zote za  nyimbo hizo na  sio ivyo tu pia alisema kuwa kwa kipindi  hiki wanataka kuwa wakazi wa arusha zawadi ya kuwaletea wasanii wote wa bendi hiyo ambapo alisema wapo 32  na wote watafika jijini Arusha

Chanzo :libeneke la kaskazini blog

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO