Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TASWIRA: RAIS KIKWETE AKIZINDUA STUDIO MPYA ZA AZAM TV JIJINI DAR JANA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa uzinduzi wa Studio mpya za Azam Tv zilizoko Tabata jijini Dar es salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa uzinduzi wa Studio mpya za Azam Tv zilizoko Tabata jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi wa Azam Tv Said Salim Bakhresa.

Mazungumzo.

Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara.

Naibu Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited, Tido Mhando.

Mhando mwenye uzoefu wa kuongoza Kampuni za vyombo vya habari zikiwemo idhaa ya Kiswahili BBC, Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) na Mwananchi Communications Limited (MCL) amesema kuwa studio hizo zina ubora kuliko nyingine zote nchini.

Jumla ya dola za Kimarekani milioni 31 (zaidi ya sh. Bilioni 56 za Tanzania) zimetumika kutengeneza studio mpya za kisasa za Azam Tv, zilizopo eneo la Tabata jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Tv Rhys Torrington.

Mc wa uzinduzi ni Taji Liundi.

Jicho la kamera.

Mwanamuziki Barnaba akiburudisha.

Wageni waalikwa.

Eneo la tukio meza kuu na wageni waalikwa.

Sehemu ya studio mpya za Azam Tv zilizoko Tabata jijini Dar es salaam.

 

PICHA ZA KWANZA KWA HISANI YA G SENGO BLOG NA PICHA ZIFUATAZO NI KUTOKA IKULU DAR ES SALAAM

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe akiwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara pamoja na uongozi na baadhi ya wafanyakazi wa Azam TV wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam leo Machi 6, 2015.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitangaza rasmi kuzinduliwa kwa studio mpya za stesheni ya Azam TV Tabata Relini jijini Dar es salaam leo Machi 6, 2015. Pamoja naye kwenye kilinge cha utangazaji ni mmiliki wa stesheni hiyo Bw. Saidi Salim Bakhressa

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Naibu Mkurugenzi wa Azam TV Bw. Dunstan Tido Mhando wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam leo Machi 6, 2015.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara pamoja na uongozi na baadhi ya wafanyakazi wa Azam TV wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam leo Machi 6, 2015.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo kutoka kwa fundi mitambo Mkuu wa Azam TV Bw. Mehdoub al Hadad juu ya namna gari la kurusha matangazo nje ya studio (OB Van) linavyofanya kazi wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam leo Machi 6, 2015.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara wakitmbezwa sehemu mbali mbali za Azam TV na mwenyeji wao Bw. Saidi Salim Bakhressa wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam leo Machi 6, 2015.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokewa na Bw. Saidi Salim Bakhressa wakati alipohudhuria sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam leo Machi 6, 2015.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokewa na Bw. Saidi Salim Bakhressa wakati alipohudhuria sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam leo Machi 6, 2015.

​PICHA NA IKULU​

 

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO