Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mbunge wa Viti Maalumu (CUF), Amina Mwidau amerithi mikoba ya Zitto kuongoza PAC

pic zitto pacMbunge wa Viti Maalumu (CUF), Amina Mwidau amerithi mikoba ya aliyekuwa mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe baada ya kuteuliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa kamati ya Hesabu za Serikai(PAC).

Kabla ya kujiuzulu ubunge Ijumaa iliyopita, Zitto alikuwa mwenyekiti wa kamati hiyo.

Kwa mujibu wa habari zilizopatikana, uchaguzi huo ulifanyika jana mchana katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

Chanzo cha habari, kimesema nafasi hiyo iligombewa na mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Lucy Owenya ambaye aliambulia kura mbili kati ya 17 zilizopigwa katika uchaguzi huo

 

Stori Kamili HAPA

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO