Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MAHAKAMA KUU YAFUTILIA MBALI KESI ILIYOFUNGULIWA NA ZITTO KABWE

 

kabwe

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imeifutilia mbali kesi iliyofunguliwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe dhidi ya Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), baada ya kukubali mapingamizi yaliwasilishwa na chama hicho.

Uamuzi huo umetolewa na Jaji Richard Mziray baada ya kupitia hoja za pande zote mbili kuhusu mapingamizi ya CHADEMA.

Mapema Saa 3:20 asubuhi Jaji Mziray alisoma uamuzi huo mbele ya wanaodaiwa kuwa wanachama huku upande wa Zitto akiwa hana mwakilishi na alikuwepo wakili wa utetezi Peter Kibatala.

Alisema baada ya kupitia hoja za pande zote mbili mahakama imeona Zitto alikosea kuifungua kesi hiyo katika Masijala Kuu ya Mahakama Kuu badala ya Masijala ya Kanda ya Dar es Salaam ya mahakama hiyo.

Pia, Zitto hakuonyesha kwa sababu gani alifungua kesi hiyo ya madai Mahakama Kuu badala ya Mahakama ya Hakimu Mkazi kama Sheria ya Mwenendo wa Kesi za Madai.

Awali mahakamani hapo CHADEMA kupitia mawakili wake kiliwasilisha kwa njia ya maandishi mapingamizi dhidi ya kesi hiyo iliyofunguliwa na Zitto.

Katika pingamizi la kwanza, CHADEMA ilidai kwamba haikuwa sahihi kesi kufunguliwa Mahakama Kuu kwa sababu ilipaswa kufunguliwa Mahakama ya Wilaya/ Hakimu Mkazi kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Kesi za madai.

Pingamizi jingine, kesi hiyo ilikosewa kufunguliwa Mahakama Kuu, Masijala Kuu badala ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Jaji alikubali mapingamizi hayo kwamba yako sahihi na kuitupilia mbali kesi hiyo.

“Mahakama inaamuru Zitto kukilipa CHADEMA gharama zote za kesi hii” alisema Jaji Mziray.

Mapema Januari 2, mwaka 2014 Mahakama Kuu, iliyoketi chini ya Jaji John Utamwa, ilitoa zuio la muda kwa Kamati Kuu ya CHADEMA, kutojadili uanachama wa Zitto katika kikao cha chake kilichofanyika Januari 3, mwaka jana.

Hata hivyo, Januari 3, mwaka 2014 mahakama hiyo ilisikiliza hoja za mawakili wa pande zote mbili kuhusu maombi hayo mbele ya Jaji John Utamwa.

Januari 7, mwaka 2014, mahakama hiyo pia ilitoa amri kwamba Zitto asijadiliwe uana chama wake hadi kesi ya msingi itakaposikilizwa na kutolewa maamuzi.

Zitto alikuwa anatetewa na wakili msomi, Albert Msando na CHADEMA walikuwa wanawakilishwa na Tundu Lisu na Peter Kibatala.

Katika kesi ya msingi, Zitto amefungua kesi dhidi ya Baraza la Wadhamini la Chama hicho na Katibu Mkuu, Willbrod Slaa, akiiomba Mahakama itoe zuio la muda la Kamati Kuu kutojadili suala la uanachama wake hadi kesi ya msingi itakaposikilizwa na kutolewa maamuzi na mahakama hiyo.

Katika maombi yake, Zitto anaiomba mahakama kuiamuru kamati kuu na chombo chochote kisijadili uanachama wake hadi rufaa yake itakaposikilizwa katika Baraza Kuu la Chama.

Kadhalika, anaoimba mahakama imwamuru, Dk. Slaa kumkabidhi nakala za taarifa na mwenendo mzima wa vikao vilivyomvua uongozi ili akate rufaa katika ngazi ya juu ya chama hicho.

Zitto kupitia wakili wake Msando aliomba mahakama itoe zuio la muda la Kamati Kuu na vikao vingine vya chama kutojadili suala la uanachama wake hadi kesi ya msingi itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.

Akiwasilisha hoja zake wakili Msando aliomba zuio hilo litolewe hadi Zitto atakapopata nafasi ya kuwasilisha rufaa yake ya kupinga uamuzi wa kumvua uongozi katika chama, uliotolewa katika kikao kilichofanyika Novemba 12 mwaka 2013.

Wakili alidai endapo amri hiyo haitatolewa na Kamati Kuu ikamvua uanachama, Zitto atapata athari kubwa kuliko chama chenyewe kwa kuwa atapoteza nafasi yake ya ubunge na kushindwa kuwatumikia wananchi waliomchagua.

Pia, mwanasheria huyo alidai athari nyingine ni kwamba iwapo atafukuzwa uanachama, Zitto atapoteza nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).

Alisisitiza kuwa, Zitto haizuii CHADEMA kufanyakazi zake za kisiasa kama wao wanavyodai katika hati ya kiapo kinzani, bali anaomba Kamati Kuu isijadili suala lake la uanachama mpaka uamuzi utakapotolewa.

Akijibu hoja hizo Wakili wa CHADEMA, Lissu alidai kuwa katika kutoa zuio la muda mahakama inatakiwa iangalie maslahi ya walio wengi na si faida ya watu wachache.

Alidai katika hati ya kiapo, Zitto anadai hakuna tarehe ya kikao cha Baraza Kuu la chama kilichopangwa, pia asipokata rufaa hatotendewa haki na atapata madhara lakini dawa ya woga na hofu yake ni kuomba mahakama iamuru kikao cha Baraza Kuu kifanyike na siyo kuomba zuio.

Lissu alidai kuvuliwa uanachama kwa Zitto hakutakuwa na athari kubwa kama anavyodai, athari ataipata yeye kwa kukosa posho na mishahara.

 

CREDIT: CHADEMA BLOG

Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO