Mgeni Rasmi wa Kongamano la tatu la Viongozi Vijana wa Afrika na China, Rais wa Zimbabwe,Robert Mugabe akihutubi usiku huu kweye kongamano hilo kwenye moja ya ukumbi wa mikutano katika hotel ya Ngurdoto mjini Arusha.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza usiku huu kwenye moja ya ukumbi wa mikutano katika hotel ya Ngurdoto mjini Arusha,ambapo Kongamano la tatu la Viongozi Vijana wa Afrika na China linafanyika na mgeni rasmi ni Rais wa Zimbabwe,Robert Mugabe.
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe (aliyeshikwa mabepa) akiwasili usiku huu kwenye moja ya ukumbi wa mikutano katika hotel ya Ngurdoto mjini Arusha,kwa ajili ya kufungua kufungua Kongamano la tatu la Viongozi Vijana wa Afrika na China.
RAIS Jakaya Kikwete akipewa tunzo ya Heshima ya juu ya Kuhamasisha Amani na Utulivu katika Bara la Afrika na Rais wa Umoja wa Vijana Afrika (PAYU),Francine Furaha Muyumba .Tuzo hiyo imetolewa na Umoja wa Vijana wa Umoja wa Afrika,pichani kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mh.Mboni Mhita
Rais Jakaya Kikwete akitoa salamu zake kwa washiriki wa Kongamano la tatu la Viongozi Vijana wa Afrika na China,ambalo mgeni rasmi ni Rais wa Zimbabwe,Robert Mugabe.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na baadhi ya washiriki wa Kongamano la tatu la Viongozi Vijana wa Afrika na China,ambapo mgeni rasmi ni Rais wa Zimbabwe,Robert Mugabe,kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana
Rais Jakaya Kikwete akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana alipowasili jioni ya leo kwenye moja ya ukumbi wa mikutano katika hotel ya Ngurdoto mjini Arusha,kwa ajili ya kutoa salamu kwa washiriki wa Kongamano la tatu la Viongozi Vijana wa Afrika na China,ambalo mgeni rasmi ni Rais wa Zimbabwe,Robert Mugabe. Pichani kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Mh.Stephen Masele.
Makamu wa Rais Dk Gharib Bilal akizungumza jambo na Rais wa Zimbambwe,Mh.Robert Mugabe mara mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa KIA,mapema leo mchaa.Rais Mugabe anatarajiwa kufungua Kongamano la Viongozi Vijana wa Afrika na China litakaloanza leo mjini Arusha.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiteta jambo na Rais wa Zimbabwe,Mh.Robert Mugabe mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa KIA mapema leo mchana.Rais Mugabe anatarajiwa kufungua Kongamano la Viongozi Vijana wa Afrika na China litakaloanza leo mjini Arusha..
0 maoni:
Post a Comment